Kuna UTAPELI mpya umeingia Nchini, kuna watu ambao wanajifanya wana
makampuni na wanatafuta watu wa kazi namaanisha wanatangaza nafasi za
kazi, nafasi hizo za kazi huzitangaza kupitia mitandao ya Internet
ambayo huwa ina maeneo ya kutangaza nafasi za ajira, nitashindwa kuitaja
mitandao hiyo kwa kuwa sio utaratibu ila wewe ambaye unajua kuwa kuna
mitandao ambayo inatangaza ajira kupitia njia ya Internet ujue ndio hiyo
ambayo tunaiongelea hapa.
Matukio yenyewe yanakuwaje: Watu hao hutangaza nafasi za kazi mbali
mbali kupitia mitandao hiyo kwa kuandika wana makampuni na wanatafuta
watu kwa nafasi mbambali kwenye makampuni yao feki, kwa kutambua
watanzania wengi wana shida ya ajira hutangaza nafasi ambazo wanaamini
wengi wataziomba na kuweka vigezo vya chini sana hasa eneo la Elimu na
uzoefu kwa kuamini wengi wataomba, baada ya hapo, wewe mwenye shida ya
ajira ukishatuma CV yako ambayo itakuwa pia inaonyesha mawasiliano yako,
wao hutumia mwanya huo kukutumia ujumbe mfupi (SMS) na kujifanya wao ni
wafanyakazi wa kampuni husika ambayo imetangaza nafasi hiyo na kujidai
wanaweza kukusaidia kuipata kazi hiyo na kukutaka uwatumie hela ili
wakufanyie mpango na kukutumia maswali ambayo utaulizwa kwenye INTERVIEW
na majibu yake, hawa jamaa kwa kutambua shida ya Watanzania hawasemi
wanataka kiasi kikubwa huwa wanataka kiasi cha Elfu kumi hadi Hamsini,
wanafanya hivyo kwa kutambua wewe mtafuta ajira unaweza ukakipata kiasi
hicho.
Matapeli hao hudiriki kukwambia na kiasi cha mshahara ambao
utalipwa kwenye kazi hiyo ili kukutamanisha utume hiyo hela, simu hiyo
ambayo imekutumia ujumbe huo ukiipigia huwa haipatikani na ikipatikana
haipokelewi na wanakua wameziregister kwa majina ambayo wanakuaminisha
ni yao kumbe ni majina ya uongo ya kutapelia watu.
Mpaka sasa wameshawaliza watu wengi sana kwa hiyo wewe mdau kuwa
makini sana wakati unaomba ajira kupitia mitandao mbalimbali ya
Internet, ukiona unaombwa hela baada ya kuomba ajira kupitia mitandao
hiyo ujue ndio hao matapeli.
KUWA MAKINI EWE MTANZANIA
IMETOLEWA NA:
MDAU MPENDA HAKI
No comments:
Post a Comment