Marehemu James Kombe.
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Aliyewahi
kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi (SACP) mstaafu James Kombe amefariki dunia wakati akipatiwa
matibabu katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
kifo hicho Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi (SSP) Advera Senso alisema, Kombe alifariki Oktoba 22 mwaka huu
na taratibu za mazishi zinaendelea.
Aidha
Senso alisema Marehemu Kombe alizaliwa mwaka 1950 huko Mwika mkoani
Kilimanjaro na alijiunga na Jeshi la Polisi tarehe 15 mwezi machi mwaka
1970 baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1969 nchini Uganda
ambapo alipandishwa vyeo na kupewa madaraka mbalimbali.
Baadhi
ya vyeo alivyopitia na miaka ya kupata vyeo hivyo katika mabano ni
pamoja na Sagenti wa Polisi (1973) Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1977),
Mkaguzi wa Polisi (1984), Mrakibu Msaidizi (1986), Mrakibu wa
Polisi(1991), Mrakibu Mwandamizi (1995), Kamishna Msaidizi wa Polisi
(1998) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2002) hadi alipostaafu
mwaka 2010.
Baadhi
ya nafasi alizowahi kuzitumikia katika Jeshi la Polisi ni pamoja na
kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) katika wilaya za Dodoma, Tarime,
Serengeti na Arusha pamoja na Kuwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa (RPC) katika
mikoa ya Lindi, Arusha, Kigoma pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza
ghasia Tanzania na hadi anastaafu alikuwa mkuu wa kikosi cha Usalama
barabarani Tanzania.
No comments:
Post a Comment