Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza
orodha ya mwisho ya wagombea wa uchaguzi wa TFF na wa Bodi ya Ligi (TPL
Board) utakaofanyika baadaye mwezi huu.
Uchaguzi
wa Bodi ya TPL utafanyika Oktoba 25 mwaka huu wakati ule wa TFF
utafanyika Oktoba 27 mwaka huu. Kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa TPL
Board na ule wa TFF zimeanza leo (Oktoba 18 mwaka huu) zitamalizika siku moja kabla ya uchaguzi saa 10 kamili alasiri.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni amewataja wagombea kwa upande
wa TPL Board kugombea uenyekiti ni Hamad Yahya Juma (Mtibwa Sugar),
Makamu Mwenyekiti ni Said Muhammad Said Abeid (Azam). Wanaowania ujumbe
wa Bodi ya Uendeshaji ni Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) na Omary Khatibu
Mwindadi (Mwadui).
Wagombea
kwenye uchaguzi wa TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani na Jamal Emily
Malinzi (Rais), Imani Omari Madega, Ramadhan Omar Nassib na Wallace
Karia (Makamu wa Rais).
Kwa
upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kalilo Samson (Kanda namba
1- Geita na Kagera), Jumbe Odessa Magati, Mugisha Galibona, Samwel
Nyalla na Vedastus Lufano (Kanda namba 2- Mara na Mwanza), Epaphra Swai
na Mbasha Matutu (Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu).
Ali
Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali (Kanda namba 4- Arusha na
Manyara), Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo (Kanda namba 5- Kigoma
na Tabora), Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo (Kanda namba 6-
Katavi na Rukwa), Ayoub Shaibu Nyenzi, David Samson Lugenge, John
Exavery Kiteve, Lusekelo Elias Mwanjala (Kanda namba 7- Iringa na
Mbeya).
James
Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge (Kanda namba 8- Njombe na
Ruvuma), Athuman Kingombe Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee
Damoder (Kanda namba 9- Lindi na Mtwara), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart
Ernest Masima, Charles Komba (Kanda namba 10- Dodoma na Singida), Farid
Nahdi, Geofrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala) na
Twahil Twaha Njoki (Kanda namba 11- Morogoro na Pwani).
Davis
Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed (Kanda namba 12- Kilimanjaro na
Pwani), Alex Crispine Kamuzelya, Kidao Wilfred Mzigama, Muhsin Said
Balhabou na Omary Isack Abdulkadir (Kanda namba 13- Dar es Salaam).
Mbwezeleni
amewataka wagombea kufanya kampeni bila kukashfu wenzao, kwani Kanuni
ya Uchaguzi za TFF toleo la 2013 inatoa fursa kwa Kamati ya Uchaguzi
kuwaondoa wagombea wa aina hiyo kwenye uchaguzi.
MAGARI MAALUMU TU MECHI YA SIMBA, YANGA
Magari
yenye shughuli maalumu tu ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanja wakati
wa mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa keshokutwa (Jumapili) kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
itaanza saa 10 kamili jioni, na kila timu inaruhusiwa kuingia na magari
matatu tu; gari la timu na mengine mawili ya viongozi. Ukaguzi wa
kuingia uwanjani ni kwa watu wote, kwani utaratibu huo si wa
kumdhalilisha mtu bali lengo lake ni kuhakikisha usalama.
Vilevile
watu hawataruhusiwa kuingia uwanjani na mifuko ya aina yoyote ikiwemo
mabegi, isipokuwa kwa waandishi wa habari wanaotumia mabegi hayo kwa
ajili ya kubebea kamera zao. Pia hakuna wafanyabishara watakaoruhusiwa
kufanya biashara katika maeneo yanayozunguka uwanja.
Kwa
washabiki watakaokuwa katika mazingira ya kuwa kero kwa wenzao wakiwemo
walevi hawataruhusiwa kuingia uwanjani, pamoja na wale wenye silaha
kama bastola ambapo wakikamatwa wafikishwa polisi na baadaye kufunguliwa
mashtaka kortini.
Barabara
ya Uwanja wa Taifa itafungwa kuanzia saa 2 asubuhi upande wa
Chang’ombe, hivyo washabiki wanatakiwa kununua tiketi zao mapema kesho
(Jumamosi) ambapo zitaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali kuanzia saa 4
asubuhi.
Vituo
hivyo ni mgahawa wa City Sports Lounge, Shule ya Sekondari Benjamin
Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora,
Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa
Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama na BMM Salon iliyoko
Sinza Madukani.
MBEYA CITY, JKT RUVU UWANJANI VPL
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kutimua vumbo kesho (Oktoba 19 mwaka
huu) kwa mechi tano huku Mbeya City ikiikaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
nyingine zitakuwa kati ya Oljoro JKT na Azam (Uwanja wa Sheikh Kaluta
Amri Abeid, Arusha), Mtibwa Sugar na Mgambo Shooting (Uwanja wa Manungu,
Turiani), Ashanti United na Ruvu Shooting (Azam Complex Chamazi, Dar es
Salaam) na Kagera Sugar dhidi ya Coastal Union (Uwanja wa Kaitaba mjini
Bukoba).
Wakati
huo huo, Ligiu Daraja la Kwanza (FDL) nayo inaendelea katika viwanja
nane kesho (Oktoba 19 mwaka huu) huku Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Dar es Salaam ukiwa mwenyeji wa mchezo kati ya African Lyon na Friends
Rangers.
Nayo
Villa Squad itacheza na Green Warriors katika Uwanja wa Mabatini,
Mlandizi, Polisi Morogoro na Kimondo (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro),
Lipuli na Kurugenzi (Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa) na
Mkamba Rangers dhidi ya Majimaji (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro).
Toto
Africans na Mwadui (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Polisi Dodoma na
Polisi Tabora (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), wakati Polisi Mara na pamba
zitacheza kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment