Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Njombe jioni ya leo,
Alhamisi, Oktoba 17, 2013, kuanza ziara ya wiki moja kukagua na kuzindua miradi
ya maendeleo katika Mkoa wa Njombe.
Miongoni mwa shughuli kubwa ambazo
Rais Kikwete atazifanya katika ziara hiyo, ya kwake ya kwanza tokea Njombe
kutangaza kuwa Mkoa, ni kuuzindua rasmi Mkoa huo.
Katika siku yake ya kwanza kesho,
Ijumaa, Oktoba 18, 2013, mbali na kuzindua Mkoa wa Njombe pia atazindua Kiwanda
cha Chai katika eneo la Ikanga na kuzungumza na wananchi.
Katika ziara hiyo ambako Rais
Kikwete atatembelea wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Njombe, Wanging’ombe,
Ludewa na Makete, pia atazindua Chuo cha Veta cha Mkoa.
Aidha, Rais atatembelea na kupata
taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wa chuma wa Liganga.
No comments:
Post a Comment