Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sifuni Mchome,(katikati) akizungumza na waandishi (hawapo pichani) Dar es Salaam jana kuhusu kufanyika kwa mtihani wa Kidato cha pili nchini kuanzia Oktoba 7hadi 21 mwaka huu.Mwengine ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shule,Marystella Wassena (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ntambi Bunyazy.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sifuni Mchome na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shule,Marystella Wassena.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sifuni Mchome na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shule,Marystella Wassena.
Baadhi ya Viongozi wa Wizarani.
Baadhi ya Viongozi Wizarani wakifuatilia jambo wakati wa Mkutano na Waandishi (hawapo pichani)
Baadhi ya Viongozi Wizarani wakifuatilia jambo wakati wa Mkutano na Waandishi (hawapo pichani).
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA
UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA PILI, 2013
1.0Utangulizi
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili kwa mwaka
2013 unatarajiwa kufanyika nchini kote kuanzia tarehe 07/10/2013 hadi tarehe
21/10/2013. Idadi ya shule/vituo vilivyosajili watahiniwa mwaka 2013 ni 4,437
ikiwa ni ongezeko la vituo 140 sawa na asilimia 3.3 ikilinganishwa na vituo
4,297 vilivyosajiliwa mwaka 2012.
2.0Watahiniwa
Jumla ya watahiniwa 531,457 wamejiandikisha
kufanya mtihani huu. Kati yao wasichana ni 270,734 (sawa na asilimia 50.9) na
wavulana ni 260,723 (sawa na asilimia 49.1). Aidha, watahiniwa waliojiandikisha
wanajumuisha makundi mawili yenye mahitaji maalum. Makundi hayo ni watahiniwa wenye uoni hafifu ambao jumla yao
ni 89 na wasioona 93. Karatasi za mtihani wa watahiniwa wenye mahitaji maalum
zimeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji yao kama vile kutumia karatasi za
“Braille” kwa wasioona na kuongeza ukubwa wa maandishi kwa wenye uoni hafifu.
3.0Umuhimu wa Mtihani wa Kidato
cha Pili
Mtihani wa Kidato cha Pili kama ilivyo
mitihani mingine ya taifa ni muhimu kwa kuwa:
·
Unapima kiwango cha maarifa na
ujuzi alioupata mwanafunzi kutokana na mada alizojifunza katika kidato cha
Kwanza na cha Pili.
·
Ni sehemu ya tathmini endelevu
katika masomo ya elimu ya sekondari.
·
Unawezesha Wizara na wadau wa
elimu kuona umahiri wa Wanafunzi katika masomo mbalimbali.
·
Unatoa changamoto zinazosaidia
wanafunzi, walimu, wizara na wadau wote wa elimu kutambua mapungufu yaliyopo
katika suala zima la ufundishaji na ujifunzaji ili yaweze kufanyiwa marekebisho
kwa lengo la kuboresha elimu.
Pamoja
na mtihani huu, Wizara inasisitiza wanafunzi kuongeza juhudi na kujituma katika
kujifunza,, kuzingatia maadili, kujenga uadilifu katika masomo yao na kujenga
utamaduni wa kusoma vitabu.
Aidha,
walimu, wazazi na walezi wanaombwa kuendelea kuwasaidia na kuwaandaa vema
wanafunzi ili wafanye mtihani katika hali ya utulivu. Vile vile wizara
inasisitiza jamii kushiriki kwa ukamilifu katika kukamilisha mahitaji ya
wanafunzi na kuweka mazingira ya shule yawe ya rafiki, bora na stahiki ili
kufanikisha zoezi zima la upatikanaji wa Elimu Bora.
Pamoja
na changamoto mbalimbali nawaasa wanafunzi wa kidato cha pili kwamba hii ndiyo
fursa yao kulionyesha taifa kuwa wanaweza, wanasoma na wanaimarika kielimu,
maarifa na ujuzi. Ari yenu iwe “kama
wengine waliweza; hata sisi tunaweza na tutafaulu” suala la kushindwa
lisiwe sehemu ya ari yenu katika mtihani huu.
4.0Hitimisho
Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaagiza Wadau wote wa elimu katika Kanda,
Manispaa na Halmashauri za Wilaya pamoja na Wazazi kuhakikisha kuwa wanafunzi
wote waliojiandikisha kufanya mtihani wanafanya
mtihani bila kukosa na katika hali
ya utulivu.
Nawatakia watahiniwa wote wa mtihani wa Kidato
cha Pili kila la heri, utulivu na mafanikio katika mtihani wao. Tunawajali na
tunawathamini na tutaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili mpate elimu, maarifa
na ujuzi ili kushiriki vyema na kwa ufanisi katika ujenzi wa taifa letu.
Mwisho kabisa niwapongeze wamiliki wa shule
yaani TAMISEMI na TAMONGSCO pamoja na walimu kwa kazi mliyoifanya kuwaandaa
wanafunzi hawa na sasa wanakaribia kufanya mtihani wa kidato cha pili.
Tuendelee kushirikiana. Tunazitambua changamoto na tutaendelea kuzishughulikia
kwa pamoja ili elimu yetu iimarike.
Prof. Sifuni E. Mchome
Katibu
Mkuu
Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
02/10/2013
No comments:
Post a Comment