KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Saturday, October 12, 2013

SHULE YA MSINGI TUNGI KIGAMBONI MANISPAA YA TEMEKE MKOA WA DAR ES SALAAM ILIYOANZA MWAKA 1975 INA MATATIZO MENGI SANA YAKIWEMO YA NYUMBA ZA WALIMU, UZIO UNAOZUNGUKA SHULE, VYOO VYA WALIMU NA WANAFUNZI, MADAWATI,MADARASA NA MENGINEYO LUKUKI.

Uzio wa magogo ya mnazi na majani makavu ndiyo yanayozunguka katika shule ya Msingi Tungi Kigamboni Dar es Salaam Manispaa ya Temeke,Shule hii ilianza mwaka 1975 mpaka sasa ina walimu 38 wanafunzi  1527 kabla ya kuondoka darasa la saba,Tatizo la Nyumba za walimu ipo moja na nyingine haijamalizika Manspaa imeshindwa kuimaliza,Vyumba vya kufundishia havitoshi,Madawati hayatoshi. 
 Miti mkavu unatumika kama sehemu ya Uzio shule inatumika kupitwa kila eneo na watu kwa kukosa uzio imara.
 Uzio unaopakana na njia kubwa inayotumika na watu mbalimbali kupitwa.
 Uzio unaopita katika nyumba ya mwalimu ambayo haijaisha kwa miaka mingi baada ya Manispaa ya Temeke kushindwa kuimalizia ujenzi.
 Mwl Mkuu Hellen Kweba Maugo (aliyesimama akizungumza) wakati wa Mahafali ya 12 ya wahitimu wa darasa la saba(7)
 Sehemu ya walimu Mkuu Msaidizi Asia Kagete(mwenye kiremba) akiwa na wengine.
 Mratibu wa Elimu Kata ya Tungi,Ester Abel Mkumbo (kulia) na mwenyekiti wa kamati ya ShuleThabiti Juma (shati drafti) pamoja na walimu.
 Mwl Mkuu  Hellen Kweba Maugo na Mratibu wa Elimu Kata ya Tungi,Ester Abel Mkumbo(kushoto)
 Mratibu wa Elimu Kata ya Tungi,Ester Abel Mkumbo,akizungumza wakati wa Mahafali.
 Darasa ambalo moja ya madawati kama yanavyoonekana katika picha hii.
 Haya ndiyo madawati ndani ya moja ya darasa.
 Hawa ni sehemu ya wahitimu 181 wa darasa la saba (7) wakifuatilia jambo.
Mwanafunzi bora toka darasa la kwanza hadi la saba Arif Juma Khamisi(kushoto) akipokea akimpa mkono mwl Mku baada ya kupokea zawadi ya kufanya vizuri katika masomo wakati wote alipokuwepo shuleni hapo.
 Nyumba ya walimu ambayo haijamalizika kwa kipindi kirefu lawama kwa Manispaa ya Temeke.
 Nyumba moja ya walimu ambayo inakaliwa na mwalimu mmoja kati ya 38.
 Wanafunzi wakinesha umaili wao katika Sarakasi wakati wa Mahafali ya 12 shuleni hapo.

 Wahimu wa darasa la saba(7) wakicheza Kwaito wakati wa Mahafali.
Sehemu ya Wazazi waliofika katika Mahafali ya 12.

KWA UFUPI
Shule hii ya Msingi Tungi Kigamboni Manispaa ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam ilianza mwaka 1975 toka hapo mpaka leo haima uzio kama picha zinavyoonesha.

Sasa ina idadi ya walimu 38 na wanafunzi 1527 kabla ya kuondoka darasa la saba mwaka huu,matundu ya vyoo 10  vinavyotumika kwa walimu na wanafunzi, nyumba ya walimu iliyo tayari moja tu na nyingine imeshindwa kukamilika kwa sababu Manispaa hajatilia mkazo kumalizika kwa nyumba hii.

Wazazi wengi hawajiwezi pia kuna fununu ya kuchukuliwa na Mwekezaji eneo la Kigamboni basi sababu hiyo inawakatisha tamaa ya kuchangia fedha kwa kuwa watapoteza,wazazi na wanakosa imani.

WITO-Mashirika ya Kibenki,Kimataifa,Watu binafsi na Tahasisi mbalimbali jitokezeni kuokoa jahazi la Elimu katika shule hiyo kwa kuwatatulia matatizo yanayowakabili Walimu na wanafunzi waliokuwepo hapo.
Kama umeguswa na Shida hizi wanazozipata katika shule hiyo na kwa msaada wa hari na Mali.Mpigie simu Mwl Mkuu.

Hellen Maugo-0783 438 700.   

No comments: