Usajili
wa wachezaji kwa dirisha dogo kwa msimu wa 2013/2014 Tanzania Bara
unafunguliwa Novemba 15 mwaka huu na utafungwa rasmi Desemba 15 mwaka
huu.
Kwa
mujibu wa kanuni, klabu zenye fursa ya kusajili wachezaji katika
dirisha dogo ni zile ambazo hazijatumia nafasi zote 30 za wachezaji.
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimemaliza duru la
kwanza msimu huu. Duru za pili litaanza kutimua vumbi Januari mwakani.
Kwa
mujibu wa Kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) matukio ya Novemba na Desemba ni dirisha dogo la usajili na mechi
za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA
Date.
Matukio
mengine ni michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye
umri chini ya miaka 20 wa klabu za VPL na michuano ya Kombe la Chalenji
itakayofanyika Nairobi, Kenya.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment