Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa
ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kenya (Harambee Stars)
itakayochezwa Jumanne, Novemba 19 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kikosi
hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager, na wengine 16 kutoka Future Taifa Stars.
Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9 mwaka huu na
kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.
Wachezaji
walioitwa ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga),
Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni
Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga),
Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi
(Azam).
Viungo
wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC
Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya
Morogoro.
Viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga),
Haruna Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba),
Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian
(Simba).
Viungo
washambuliaji ni Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho
Ngasa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji
ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa SugarMbwana Samata
(TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment