1.0
UTANGULIZI
Mfuko
wa Akiba GEPF ulianzishwa chini ya sheria Namba 51 ya mwaka 1942 iliyofanyiwa
marejeo mwaka 2002 (Re 2002). Madhumuni ya Mfuko hapo awali ilikuwa kutoa huduma
ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa serikali kuu ambao utumishi wao ilikuwa si wa masharti ya kudumu na malipo ya
pensheni. Mfuko huu toka kuanzishwa mwaka 1942 ulifanya kazi zake chini ya
Wizara ya Fedha mpaka kufikia mwaka 2004 ambapo Mfuko ulipata Bodi yake na Menejimenti
na kuanza kufanya kazi kama taasisi ya umma inayojitegemea.
Dira ya Mfuko
Kujenga
Mfuko wenye wigo mpana wa wanachama na wenye kutoa huduma zinazokidhi matarajio
ya wanachama
Dhima ya Mfuko
Kutoa kwa wakati mafao bora
yanayokidhi matarajio ya wanachama kwa kutumia teknolojia ya habari na
mawasiliano ya kisasa na watumishi wenye uwezo na ari ya kujituma
2.0 HALI YA MFUKO MWAKA 2004
Wanachama - 16,131
Michango - 5.12
(Sh) Bilioni;
Mafao
- 67.10 (Sh) Milioni
Vitega
uchumi - 17.98 (Sh) Bilioni
Thamani
ya Mfuko- 20.21
(Sh) Bilioni
3.0 HALI YA MFUKO 2012/13
Wanachama 62,256
Michango 37.2 Bilioni
Mafao 9.5 Bilioni
Vitegauchumi 179.5 Bilioni
Thamani 198.38 Bilioni
4.0
MABADILIKO
YA MFUMO WA UENDESHAJI TOKA AKIBA KWENDA PENSHENI
Bunge
la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limepitisha sheria mpya ya Mfuko wa GEPF
ambayo pamoja na mambo mengine inabadili mfumo wa uendeshaji na kuruhusu GEPF
kulipa mafao ya muda mrefu (Pensheni).
Sheria hii mpya imezingatia sheria ya SSRA sheria namba 5 ya mwaka
2012. Mafao mapya yatakayolipwa na GEPF
ni pamoja na:
Fao la Msaada wa Mazishi
Fao la pensheni
Fao la Elimu
Fao la Kufariki Kazini
5.0
MPANGO
WA HIARI WA KUJIWEKEA AKIBA YA UZEENI (VSRS)
Hii
ni Skimu maalum ambayo imebuniwa mwaka 2009 ili kutoa fursa kwa watu wote
kuweka akiba ambayo itawasaidia kupambana na majanga mbalimbali ikiwemo uzee.
Mpango huu ni matokeo ya mageuzi katika sekta ambayo yanamtaka kila mtu mwenye
uwezo wa kuzalisha kipato anaweza kujiunga na Hifadhi ya Jamii. Kupitia Skimu
hii kila mtu anaweza kujiunga, awe mkulima, mjasiliamali, sekta ya usafiri na
makundi mengine.
Mafanikio
katika Skimu ya Hiari (VSRS)
Usajili wa wanachama wamefikia – 18,050
Akiba za wanachama zimefikia – TZS 3.1 Bilioni
Matarajio kufikia June
2014
Wanachama – 33,226
Akiba za wanachama – TZS
5.10 bilioni.
Mkurugenzi wa Masoko na Uendeshaji wa Mfuko wa Malipo ya Kustaafu wa GEPF,Anselini Peter (kulia) akizungumza na waandishi (hawapo pichani) Dar es Salaam jana kuhusu mafanikio makubwa wanayoyapata hivi sasa.Mwengine Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja,Aloyce Ntukamazina.
Mkurugenzi wa Masoko na Uendeshaji wa Mfuko wa Malipo ya Kustaafu wa GEPF,Anselini Peter (kulia) akizungumza na waandishi (hawapo pichani) Dar es Salaam jana kuhusu mafanikio makubwa wanayoyapata hivi sasa.Mwengine Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja,Aloyce Ntukamazina.(Na Tanzania Live Blog).
No comments:
Post a Comment