KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Saturday, November 16, 2013

MWILI WA DKT, SENGONDO MVUNGI,WAAGWA NA MAELFU YA WATU VIWANJA VYA KALIMJEE DAR ES SALAAM,KUZIKWA KILIMANJARO JUMATATU.

 Baadhi ya wanachama wa Chama cha NCCR –Mageuzi wakibeba sanduku lililofunikwa na bendera ya Chama lillohifadhiwa mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Katiba,Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho na Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya ,Dkt Sengondo Mvungi,ukiwasilishwa katika Viwanja vya Kalimjee Dar es Salaam jana tayari kwa kutolewa heshima za mwisho na kuagwa kabla ya kusafirishwa leo mkoani Kilimanjaro kwa mazishi kesho.
Viongozi wa Dini wa Kanisa Katoliki wakiendesha Ibada katika kuuwaga mwili wa Dkt,Sengondo Mvungi.
 Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa wakiongozwa na Profesa Ibrahimu Lipumba (watatu msitari wa mbele CUF) wakifuatilia wakati wa kuaga mwili.
 Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia (kushoto) na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalimu Seif Sharif Hamad kwa pamoja wakiwa wameshika Tama kwa Uzuni.
 Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Warioba akitoa heshima za mwisho.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Saidi Ali Mwema,akitoa heshima za mwisho.
 Mawakili na watu wengine wakifuatilia kabla ya kutoa heshima za mwisho.
 Kinamama wakifuatilia jambo kabla ya kutoa heshima za mwisho.
 Kaimu Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali ya Daily News,Sunday News,Habarileo na Spotleo Gabriel Nderumaki akitoa heshima za mwisho.
 Mke wa marehemu Dkt,Sengondo Mvungi,Anna Mvungi (aliyeshikwa anajipangusa machozi) alishndwa kujizuia wakati wa kutoa heshima za mwisho.
 Mawakili wakibeba jeneza lenye mwili wa Dkt,Sengondo Mvungi.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Benjamin Mkapa, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt,Sengondo Mvungi,katika Viwanja vya Kalimjee Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt, Sengondo Mvungi.

Makamu wa Kwanza wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalimu Seif Sharif Hamad akitoa heshima za mwisho.

No comments: