Michuano
ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20
wa klabu za Ligi Kuu inaanza kutimua vumbi Novemba 17 mwaka huu katika
viwanja vya Karume na Azam Complex, Dar es Salaam.
Droo
ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Maji Uhai imefanyika leo (Novemba 8
mwaka huu) mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambapo timu zimepangwa katika makundi
matatu.
Kundi
A linaundwa na timu za Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Mbeya City
na Yanga, wakati kundi B ni Ashanti United, Mgambo Shooting, Oljoro JKT
na Ruvu Shooting. Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Rhino Rangers na Tanzania
Prisons ndizo zinazounda kundi C.
Mechi
za ufunguzi kundi A Novemba 17 mwaka huu ni kati ya Azam na Coastal
Union (saa 2 asubuhi- Karume), Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana-
Karume). Kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi-
Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10 jioni- Karume).
Kagera
Sugar na Mtibwa Sugar (saa 2 asubuhi- Azam) na Rhino Rangers na
Tanzania Prisons (saa 10 jioni- Azam) ndizo zitakazocheza mechi za
ufunguzi Novemba 17 mwaka huu katika kundi C.
Robo
fainali ya michuano hiyo itachezwa Novemba 24 na 25 mwaka huu wakati
nusu fainali itapigwa Novemba 26 na 27 mwaka huu. Mechi ya kutafuta
mshindi wa tatu na ile ya fainali zitachezwa Novemba 30 mwaka.
TANZANITE YATUA SALAMA MAPUTO
Kikosi
cha timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) kimewasili
salama jijini Maputo, Msumbiji tayari kwa mechi ya marudiano ya raundi
ya kwanza ya Kombe la Dunia itakayochezwa kesho (Novemba 9 mwaka huu).
Kwa
mujibu wa kiongozi wa msafara wa Tanzanite, Kidao Wilfred ambaye pia ni
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), timu hiyo chini ya Kocha wake Rogasian Kaijage ilifanya mazoezi
yake ya kwanza jana asubuhi.
Tanzanite
itafanya mazoezi yake ya mwisho leo (Novemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Taifa wa Zimpeto ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi hiyo
itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni kwa saa za Msumbiji.
Nao
wachezaji waliobaki kumalizia mtihani yao ya kidato cha nne wameondoka
leo saa 11 jioni kwa ndege ya LAM wakiongozwa na naibu kiongozi wa
msafara, Khadija Abdallah Nuhu ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA).
KESSY KUSIMAMIA MECHI YA KOMBE LA DUNIA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Lina Kessy kuwa kamishna wa
mechi ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kwa wanawake chini ya umri wa
miaka 20 kati ya Afrika Kusini na Botswana.
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza itachezwa nchini Afrika Kusini,
Novemba 9 mwaka huu. Waamuzi kutoka Zambia ndiyo watakaochezesha mechi
hiyo namba kumi.
Waamuzi
hao wataongozwa na Glads lengwe atakayepuliza filimbi wakati mwamuzi
msaidizi namba moja ni Bernadette Kwimbira kutoka Malawi, namba mbili ni
Mercy Zulu na mezani atakuwepo Sarah Ramadhani, wote wa Zambia.
Afrika
Kusini ilishinda mechi ya kwanza ugenini mabao 5-2. Mshindi wa mechi
hiyo atacheza raundi ya pili na mshindi wa mechi kati ya Tanzania na
Msumbiji.
MECHI YA JKT RUVU, COASTAL YAINGIZA LAKI 2/-
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji JKT Ruvu na Coastal Union
ya Tanga iliyochezwa juzi (Novemba 6 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex,
Dar es Salaam imeingiza sh. 201,000.
JKT
Ruvu iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi hiyo namba 85 na
kushuhudiwa na watazamaji 67 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh.
3,000 na 10,000.
Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 39,010 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 30,661.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 19,835, tiketi sh.
38,100, gharama za mechi sh. 11,901, Bodi ya Ligi sh. 11,901, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,950 na Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 4,628.
Nayo
mechi kati ya Ashanti United na Simba iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa
imeingiza sh. 24,931,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh.
5,333,590.
Wakati
huo huo, mechi za jana (Novemba 7 mwaka huu) kati ya Yanga na Oljoro
imeingiza sh. 34,902,000 kutokana na watazamaji 6,045 ambapo kila klabu
imepata sh. 7,812,477.95. Mechi ya Azam na Mbeya City iliyochezwa Azam
Complex yenyewe imeingiza sh. 15,973,000 kwa watazamaji 4,857 na kila
klabu imepata sh. 3,953,162.
WATATU WAOMBEWA ITC KUCHEZA UJERUMANI
Watanzania
watatu wameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na Chama cha
Mpira wa Miguu Ujerumani (DFB) ili wacheze mpira wa miguu nchini humo.
Wachezaji
hao ni Charles Mishetto na David Sondo wanaombewa hati hiyo ili waweze
kujiunga na timu ya SpVgg 1914 Selbitz, wakati Eric Magesa ameombewa
kibali hicho ili achezee timu ya klabu ya SC Morslingen.
Hata
hivyo, katika maombi hayo DFB haikuleza hapa nchini walikuwa wakicheza
katika klabu zipi. Wachezaji wote wameombewa hati hiyo kama wachezaji wa
ridhaa.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment