Na Anna Nkinda –
Colombo, Sri Lanka
Watoto wenye mahitaji maalum wanahitaji
kupata ulinzi na mapenzi ya mara kwa mara kutoka kwa walezi na jamii
inayowazunguka ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kwenda shule kwani wengi wao
wananyimwa fursa hiyo ukilinganisha na
watoto wengine.
Aidha mtoto akipata elimu ni moja ya hatua
ya mwanzo katika maendeleo ya taifa kwani baada ya kuelimika atakuwa na ujuzi wa kitaaluma, kiteknolojia na raia mwenye kufuata maadili ya nchi yake.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shule ya awali ya Carlton inayoongozwa na Mke
wa Rais wa
Sri Lanka Mama Shiranthi Wickremasinghe
Rajapaksa wakati wake wa Marais na wakuu
wa nchi na Serikali walipotembelea shule
hiyo iliyopo mjini Colombo jana ilionyesha kuwa shule hiyo inamtazamo wa kutoa elimu kwa mtoto.
Elimu ya shule hiyo
ambayo hutolewa bure kwa watoto wenye mahitaji maalum na wasio na mahitaji
maalum imebuniwa kwa nia ya pekee ya kutoa elimu sambamba na viwango vya kimataifa
kwa watoto wan chi hiyo ambao wanafundishwa kupitia njia rahisi ya nadharia na vitendo ambavyo vinamfanya mtoto aweze kuelewa zaidi.
Shule hiyo ilianza mwaka 1982 ikiwa na
wanafunzi nane ambapo Mama Rajapaksa alikuwa ni mmoja wa walimu wawili
waliokuwepo ambao waliweza kutoa elimu kwa watoto na kutokana na jitihada zake baadhi yao baada ya kumaliza masomo wameweza
kushika nyadhifa mbalimbali katika nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwakilisha Bunge la nchi.
Hasi sasa inamatawi nane yaliyopo katika
mikoa mitatu ya nchi hiyo na
kuwa na zaidi ya watoto 2000 huku ikiwa
na malengo ya kuendeleza utu wa watoto, kutoa ujuzi wa uongozi, kuwawezesha
watoto kuweza kujiamini na kujithamini, kukuza stadi za watoto, kusimamia maadili na kurejesha nidhamu kwa watoto.
Walimu wa shule hiyo hufanya kazi ya kutambua vipaji vya watoto kwani huwapa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika matamasha ya mwisho wa mwaka na hivyo kuweza kutimiza ndoto zao na kupatikana kwa viongozi wazuri katika siku za usoni.
Walimu wa shule hiyo hufanya kazi ya kutambua vipaji vya watoto kwani huwapa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika matamasha ya mwisho wa mwaka na hivyo kuweza kutimiza ndoto zao na kupatikana kwa viongozi wazuri katika siku za usoni.
Wakiwa shuleni hapo wake hao wa marais
na wakuu wa Serikali walijionea michezo mbalimbali iliyochezwa na watoto hao wenye
umri wa chini ya miaka mitano ikiwemo ngoma, kareti na kuogelea ambayo
inawajenga kiakili na kiafya na hivyo kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.
Wake hao wa Marais na wakuu wa serikali akiwemo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete walihudhuria
mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) uliomalizika leo
nchini humo.
No comments:
Post a Comment