Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof
Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku wa
kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini
Mzee Nelson R. Mandela.(PICHA NA IKULU)
Rais
wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewasili
katika mji mkuu wa Afrika Kusini wa Pretoria usiku wa leo, Jumatatu,
Desemba 9,
2013, kuhudhuria Ibada Kuu ya Kitaifa (Memorial Service) ya msiba wa
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela kwenye Uwanja wa
Michezo wa FNB mjini Johannesburg.
Rais Kikwete
anajiunga na mamia ya viongozi wa nchi mbali mbali duniani kuomboleza kifo cha
mmoja wa viongozi mashuhuri zaidi duniani katika karne za 20 na 21.
Rais Kikwete
ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa Pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na mkewe
Mama Asha; Mama Salma Kikwete na Ndugu Abdulahramani Kinana, Katibu wa Mkuu wa CCM.
No comments:
Post a Comment