Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akipanda behewa na wasaidizi
wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro (katikati) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (juu),
wakati yeye na msafara wake waliposafiri kwa treni kwa zaidi ya saa 22,
kutoka Stesheni ya Makambako na kuwasili Dar es Salaam kwa teni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA),
mwishoni mwa ziara yake ya zaidi ya siku 25, ya kukagua utekelezaji wa
ilani ya CCM, kusikiliza kero za Wananchi na kujadiliana nao njia ya
kuzitatua, katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe. Treni
ilitoka Makambako jana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na wasaidizi wake, Katibu wa
NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati) na
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (juu), waksihuka kwenye
behewa kwenye stesheni ya Mlimba, wilayani Kilombelo mkoani Morogoro,
baada ya treni kufika kwenye stesheni hiyo jana, Des. 8, 2013,
waliposafiri kwa treni kwa zaidi ya saa 22, kutoka Makambako na
kuwasili Dar es Salaam kwa teni ya Shirika la Reli
la Tanzania na Zambia (TAZARA), mwishoni mwa ziara yake ya zaidi ya siku
25, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za Wananchi
na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma,
Mbeya na Njombe. Treni ilitoka Makambako jana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akitoka kukagua
jengo la stesheni ya lulimba mkoani Morogoro ambayo aliikagua akiwa
njiani kurejea Dar es Salaam akitokea Makambako, mwishoni mwa ziara yake
ya zaidi ya siku 25, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza
kero za Wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika Mikoa ya
Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe. Wengine ni Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mlimba wilayani
Kilombero, Selemani Balali na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinunua karanga kwa mama mmoja
aliyekuwa aliuza karanga hizo kwenye stesheni ya Mlimba, Kilombero
mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumzana baadhi ya wasafiri
aliposhuka katika stesheni ya Mlimba, wakati akisafiri kwa treni ya
TAZARA kutoka Makambako kwenda Dar es Salaam mwishoni mwa
ziara yake ya zaidi ya siku 25, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM,
kusikiliza kero za Wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika
Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe. Kushoto ni Kijana, Richard
Ambikise kutoka Makambako.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiuliza bei ya samaki kwa
Jacob Thomas, aliyekuwa akifanya biashara hiyo kwenye Stesheni ya
Mlimba, Kilombero mkoani Morogoro, jana Nape na Dk.
Asha-Rose walikuwa wameshuka kwenye stesheni hiyo wakiwa na Katibu Mkuu
wa CCM Abdulrahman Kinana ambaye alisafiri kwa trebi ya TAZARA kutoka
Makambako kwenda Dar es Sakaam, mwishoni mwa ziara yake ya zaidi ya siku
25, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za Wananchi
na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma,
Mbeya na Njombe.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Ramadhan Madabida, baada ya kuwasili stesheni ya
TAZARA mjini Dar es Salaam, alitokea Makambako, mwishoni mwa ziara yake
ya zaidi ya siku 25, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza
kero za Wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika Mikoa ya
Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro. Treni ilitoka Makambako.
Ujumbe wa Kinana ukiwasili TAZARA Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahyman Kinana na Nape wakiagana na waandishi wa habari kwa furaha, baada ya kuwasili stesheni ya TAZARA mjini Dar es Salaam, Des 9, 2013. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).
No comments:
Post a Comment