Na
Andrew Chale, Zanzibar
MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Dk.
Ali Mohammed Shein kesho Januari 26, anatrajiwa kumnadi mgombea wa
Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo, katika uchaguzi
mdogo unaoendelea kwenye jimbo hilo.
Katika tarifa yake, Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM
Zanzibar, Dk Shein atakuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa nne wa
hadhara kwenye kampeni hizo zinazoendelea.
Na kuongeza kuwa, Dk. Shein
atawahutubia wananchi sambamba na kumnadi, Mgombea huyo wa nafasi ya
uwakilishi, Mahmoud Thabit Kombo, anayewania nafasi hiyo kwenye jimbo hilo la
Kiembesamaki.
Vuai aliwataka wananchi wa jimbo
hilo kujitokeza kwa wingi ilikusikiliza sera na ilani za chama hicho katika
utekelezaji wake iliwakichague chama cha Mapinduzi kwa misingi imara ya
kuwaletea maendeleo.
Aidha, kwa upande wake,
Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wananchi wa jimbo hilo, kumpigia kura hiyo
Februari mbili, ili akawawakilishe kwenye Baraza la Wawakilishi.
“Nawaomba Wanakiembesamaki, kutumia
fursa ya kipekee ya kunichagua ilikuweza kuwawakilisha kwenye BAraza,
hakika chama chetu ni sikivu na daima kipo na wananchi katika kuwatetea
na kuwaletea maendeleo” alisema, Mahmoud.
Kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo
la Kiembesamaki, zilianza Januari 21, ambapo zinatarajia kumalizika Februari
Mosi, mwaka huu huku wananchi wakitarajia kupiga kura ya chaguzi huo, Februari
mbili.
No comments:
Post a Comment