Profesa wa uchumi anayeheshimika duniani ameusifia
uamuzi wa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete kuanzisha Benki ya Kilimo, akisema kuwa kwa karibu muongo
mzima wa jitihada za dunia kuboresha kilimo katika Afrika hakuna jambo zuri
zaidi limefanyika kama uamuzi wa kuanzisha Benki hiyo.
Mtaalam huyo, Profesa Jeffrey Sachs, amesema kuwa
pamoja na kwamba dunia imekuwa inajadili jinsi gani ya kuwasaidia wakulima
wadogo katika Afrika kuimarisha kilimo chao na hivyo kuinua kipato chao, hakuna
taasisi yoyote imechukua hatua ya maana kama ile inayochukuliwa na Serikali ya
Tanzania.
Profesa Sachs alikuwa anazungumza usiku wa juzi,
Jumatano, Januari 22, 2014, wakati wa mjadala kuhusu jinsi ya kuongeza kasi ya
mafanikio katika kilimo cha Afrika kwenye Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na
Taasisi ya Kilimo ya Grow Africa mjini Davos, Uswisi, ikiwa moja ya shughuli za
Mkutano wa Mwaka 2014 wa Taasisi ya Uchumi Duniani (WEF).
Baada ya kusikiliza hotuba za viongozi mbali zikiwamo
za Rais Kikwete mwenyewe na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mheshimiwa……………, Profesa
Sachs alisimama na kuonekana kulalamika kuwa hatua ambazo zimekuwa
zinachukuliwa na dunia kuhusu kuongeza tija katika kilimo cha Afrika zimekuwa
hazina mafanikio makubwa zaidi kwa sababu hazitoshi.
“Moja ya mambo ambayo sote tunayajua fika na
tumeyajadili sana ni ugumu wa wa mkulima wa Afrika kupata fedha, hata kidogo,
za kuwekeza katika shughuli yake….aweze kununua mbegu bora, aweze kununua
mbolea, aweze kulima kisasa, lakini mimi naona umekuwa ni mjadala zaidi kuliko
vitendo,” alisema Profesa huyo na kuongeza:
“Ndiyo maana nathubutu kusema kuwa kama kuna jambo
kubwa na la maana sana ambalo limefanyika katika muongo mzima wa mjadala kuhusu
kilimo ni uamuzi wa Serikali ya Tanzania kuanzisha benki ya umma ya kuwahudumia
wakulima. Huu ni uamuzi sahihi kabisa.”
“Hivyo, sina shaka kusema kuwa katika moja ya
mambo yaliyonivutia katika mjadala wa usiku wa leo ni uamuzi huu wa kuwa na
benki ya umma ya kilimo kwa sababu sekta bibafsi imeshindwa kulifanya jambo
hili,” alisema profesa Sachs.
Aliongeza: “Benki za kilimo za umma zilianzishwa
katika maeneo mengi huku nyuma kwa msaada wa taasisi za fedha za kimataifa.
Zilianzishwa katika nchi za Marekani, zilianzishwa Ulaya na zilianzishwa Asia
lakini ilipofika zamu ya kuanzisha benki hizo katika Afrika mpango huo
ulisimaishwa kwa sababu ambazo kwa hakika hazijapaswa kuelezwa sawasawa.
Serikali ya Rais Kikwete imeamua kuanzisha benki
ya Kilimo kwa nia ya kusaidia sekta ya kilimo na kuwezesha wakulima kupata beni
ambako wanaweza kupata mikopo kwa uhakika na urahisi zaidi.
Benki hiyo ilikuwa izinduliwe mwishoni mwa mwaka
jana lakini uzinduzi huo uliahishwa hadi mwaka huu.
No comments:
Post a Comment