Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na sasa ni Waziri wa Ulinzi
na jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) akizungumza na
watendaji wa wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya
ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri wake na sasa ameteulikuwa kushika
nyadhifa ya Uwaziri Dkt. Seif Rashid (kulia), anayefuata ni Naibu Waziri
wa Wizara hiyo Dkt. Kebwe S. Kebwe.Makabidhiano hayo yamefanyika
kwenye ukumbi wa Waziri, wizarani hapo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Seif Rashid (kulia) akizungumza
na watendaji wa wizara hiyo (hawapo pichani) na kutoa shukrani zake za
dhati kwa aliyekuwa Waziri wake Dkt. Mwinyi kwa ushirikiano wake
kipindi alipokuwa akiongoza wizara hiyo.
Naibu Waziri Dkt. Kebwe S. Kebwe akizungumza na watendaji wa wizara
hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano na mahusiano mazuri ili
kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Waziri wa Ulinzi Dkt. Mwinyi akiteta jambo na katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jami, Charles Pallangyo.
Mawaziri hao wakisaini vitabu vya makabidhiano ya Muundo na Utekelezaji wa Wizara.
Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Mwinyi (kushoto) akimkabidhi kitabu hicho Waziri Mpya wa Wizara hiyo Dkt. Seif.
Naibu Waziri Dkt. Kebwe,(kulia) akikabidhiwa kitabu na Waziri dkt. Mwinyi,(kushoto)
Mawaziri hao wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano
pamoja na watendaji wa wizara hiyo. Wa kwanza kushopto waliokaa ni
Katibu Mkuu, Charles Pallangyo, aliyekuwa Waziri wa afya na ustawi wa
jamii Dkt. Mwinyi, Waziri mpya wa wizara hiyo Dkt. Seif nna wa mwisho
kulia ni Naibu Waziri Dkt. Kebwe S. Kebwe ( Picha zote na Catherine
Sungura-MOHSW).
No comments:
Post a Comment