Mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara
unaanza kesho (Januari 25 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa katika
miji ya Bukoba, Dar es Salaam na Tanga.
Mabingwa
watetezi Yanga watakuwa wageni wa Ashanti United kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam wakati kwenye jiji hilo hilo Uwanja wa Azam Complex
kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Azam FC na Mtibwa Sugar kutoka
Morogoro.
Coastal
Union na Oljoro JKT zitaumana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga,
huku Kagera Sugar ikiikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba.
Raundi
ya 14 ya ligi hiyo itaendelea Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi
mbili. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa shuhuda wa mechi kati ya
Simba na Rhino Rangers kutoka Tabora wakati maafande wa JKT Ruvu na
Mgambo Shooting watapambana Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Viingilio
kwenye mechi ya Ashanti United na Yanga vitakuwa sh. 5,000, sh. 15,000
na sh. 20,000. Viingilio mechi ya Mkwakwani vitakuwa sh. 10,000 kwa sh.
3,000, Uwanja wa Azam Complex sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa
Kaitaba ni sh. 5,000 kwa sh. 3,000.
MECHI ZOTE TIKETI ELEKTRONIKI ISIPOKUWA TAIFA
Viwanja
vyote ambavyo tayari vimefungwa mfumo wa elektroniki vitatumia tiketi
za elektroniki isipokuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambao wenyewe
utachelewa kidogo ili kuangalia kwanza mfumo huo unavyofanya kazi katika
viwanja vingine.
Kwa
viwanja vinavyotumia mfumo huo tiketi zinanunuliwa kupitia mtandao wa
Vodacom ambapo mteja ni lazima awe amesajiliwa katika MPESA. Ataanza kwa
kupiga *150*03*02# ambapo atapewa namba ya kumbukumbu anayotakiwa
kuihifadhi kwani ataulizwa wakati anafanya malipo kwa kupitia MPESA
ambapo ataingia kama kawaida kwa kutumia *150*00#.
Baada
ya kulipa atapewa namba ya tiketi ambapo atakwenda kwenye mashine
maalumu za kuchapa (printer) ambazo ziko katika vituo mbalimbali na
kuchapa tiketi hiyo ambayo ndiyo atakayokwenda nayo uwanjani.
Njia
nyingine ya kununua ni kwa wateja wa benki ya CRDB ambayo wamejisajili
kwenye simbanking. Wao wataingia kwa kutumia *150*03# na kufanya malipo
ya tiketi. Nao baada ya kupata namba watakwenda ku-print tiketi kwenye
mashine hizo maalumu.
Vilevile
tiketi zinapatikana kupitia maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo
katika maeneo mbalimbali nchini. Watakaonunua kupitia maduka hayo
watapata tiketi na kwenda moja kwa moja uwanjani.
DAR ES SALAAM
Kwa
mechi za Dar es Salaam (Uwanja wa Azam) ambao ndiyo unaanza kutumia
tiketi za elektroniki maduka ya CRDB Fahari Huduma yanayouza tiketi hizo
ni; 1 Shs Distributors Limited (Mtoni Kwa Aziz Ally), ABC Computer
(Mtaa wa Samora), Abdi Ally Abdi (Kariakoo), Aika- El Traders
(Africana), Amaly Investment (Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo), Athuman Fakhi
Adam (Kongowe, Mbagala) na Bemuda Supplies Agency (Tegeta- Kibo
Complex).
Benedict
Traders (Barabara ya Uhuru/Lumumba), Ellytex Investment (Mtaa wa Indira
Gandhi), Fedha Investment Limited (Pamba Road), Fuya Godwin Kimbita
(Tegeta Block E), Hakika Limited (Mtaa wa Swahili, Kariakoo), Irice
Stationary (Tegea Kwa Ndevu), Joshua Andrew Kisamo (Mtaa wa Kongo,
Kariakoo), LB Pharmacy (Mtoni Kijichi) na Lista Phares Barnabas (Tabata
Segerea).
L.M.S.
Agro Chemical (Sokoni Kariakoo), Matei Laurent Kiria (Mbuyuni,
Kinyerezi), Michael Elisante Mchomvu (Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo),
Palmall General Supplies (Barabara ya Shekilango), Rafabi Communications
(Mtaa wa Livingstone, Kariakoo), Therry Inestment Limited (Tegeta
Kibaoni) na Wemerick Independent Vehicle Diagnostic Company Limited
(Mtaa wa Boko).
Mashine
za kuchapia tiketi zipo matawi ya CRDB Azikiwe, Holland House (mashine
mbili), Kariakoo, Tabata, Tegeta, Mbezi beach, Vijana na Quality Center.
Mashine nyingine maeneo ya ATM ya Mtaa wa Shaurimoyo (mbili), Kawe
Oilcom, Tabata Camel, Manzese, Ubungo Oilcom, Sabasaba na Mbagala
Oilcom.
BUKOBA
Maduka
ya CRDB Fahari Huduma ni Tak-Biir Investment Company (Mtaa wa Jamhuri,
Bilele), Mary Mother of Peace Buhembe School (Sido Block, Rwamishenye),
Muleba Secretarial Bureau (Nyerere Road), Akimu Abdallah Tirutoijwa
(Mtaa wa Forodhani), Jamila Rajabu Songoro (Mtaa wa Jamhuri, Bilele),
Rukia Kassim Mohamed (Mtaa wa Kashai, Kashenye) na Novath Michael Kibira
(Uganda Road, Majengo).
Mashine tatu za kuchapia tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Bukoba.
TANGA
Maduka
ya CRDB Fahari Huduma ni Fax Auction Mart (Sabasaba Ground, Korogwe
Road) na Rozalia Aloyce Masanja (Usagara, Block K). Mashine tatu za
kuchapia tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Tanga.
MBEYA
Maduka
ya CRDB Fahari Huduma ni Blue Bird Bureau de Change (Lupa way), Meenda
Pharmacy Limited (Maendeleo), Access Computer Limited (Lupa way,
Sisimba) na Japhes James Mwanjisi (Mtaa wa Njisi). Mashine za kuchapia
tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Mbeya (mbili), Tawi la
Mwanjelwa na Uyole.
MOROGORO
Duka
la CRDB Fahari Huduma ni Shambani Graduates Enterprises Limited
(Kihonda) na pia kutakuwa na gari za CRDB (Mobile bank). Mashine za
kuchapia tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Morogoro, Msamvu
na Morogoro Agency.
ARUSHA
Maduka
ya CRDB Fahari Huduma ni Fanuel John Andrew (Arumeru, Maji ya Chai),
Robert William Maeda (Arumeru, Usa River), Wakwetu General Supplies
(Mtaa wa Ngongongare, Arumeru), Wallace Ndawonga Mtawa (Kimandolu Suye),
Side Corner Multi Business (Levolosi, Makao Mapya Street) na Albertha
Ibrahimu General (Usa River Bus Stand).
Mashine za kuchapia tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Arusha (mbili), Tawi la Meru, TFA, TRA Mapato na Ngaramtoni.
MWANZA
Maduka
ya CRDB Fahari Huduma ni Majura General Supplies (Mecco Street), Prisca
Joachim Kitani (Gilishi Street), Niche Consult (Nyerere Road),
Deogratias Just Silayo (Malimbe, Mkolani), Yohana Ndili Mahago (Igoma
Mashariki), Emily Elias Sambo (Sweya Street), Y Financing Limited
(Kilimahewa) na Mangare Office Solutions (Station Road).
Makoye
E. Serikali (Ilemela, Kiseke Street), Elizabeth George Kiwia (Uhuru
Road), Mwalimu General Services (Kitangiri Road), George Edward Mulambo
(Pasiansi), Nginila Office Solutions (Rufiji Street), Elvando IT
Solutions (Nkrumah, Nyamagana), Sarimosa Company Limited (Kaluta Street)
na Sahara Trasport and Scrappers Dealers (Mission, Pamba Road).
Mashine
za kuchapia tiketi (printers) zipo CRDB matawi ya Mwanza, Nyerere na
Mwaloni wakati nyingine zipo Nyanza, Buzuruga na Ilemela.
ONYO KWA MAKOCHA, MAOFISA HABARI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawakumbusha makocha na maofisa
habari wa klabu za Ligi Kuu kujiepusha na kauli za chuki, uchochezi na
uongo kwa shirikisho na waamuzi kila timu zao zinapofanya vibaya kwenye
mechi.
Ni
wajibu wa makocha kuzungumzia matokeo ya timu zao kiufundi badala ya
kushambulia waamuzi na TFF kwa maneno makali. Pia maofisa habari nao
wanatakiwa kuwa makini katika kauli zao kuhusiana na matokeo na masuala
mengine.
Kwa wale watakaokwenda kinyume TFF itawafikisha kwenye vyombo vya kinidhamu na maadili kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment