Ndugu waandishi wa habari tunapenda kutambua uwepo wenu katika ukumbi
huu leo ili mpate kutusikiliza na kwa hilo tunapenda sana kuwashukuru kwa
kufika hapa mda huu. Tanzania Youth
Vision Association (TYVA) ni asasi
ya vijana isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mnamo mwanzoni mwa miaka ya 2000 na
kupata usajili wake mwaka 2002 kupitia wizara ya mambo ya ndani, Hivyo Asasi hii
haifungamani na chama chochote cha siasa, dini,ukanda ukabila, na malengo
yakuanzishwa kwake ilikuwa na malengo makuu mawili Kwanza ni kujenga jamii
huru, ya haki na ya kidemokrasia ambamo vijana wana ushiriki wa hali ya juu na
makini.
Pili bila kusahau kwa miaka hiyo
kulikuwa na ushawishi na ushiriki mdogo wa vijana katika ngazi mbalimbali za
maamuzi hivyo basi lengo pia lilikuwa ni kujaza nafasi iliyokuwa wazi ya
kukosekana kwa asasi makini yenye uwezo wa kutetea vijana katika changamoto zao
kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni, Pia kushawishi watunga sera na
wafanya maamuzi katika ngazi mbalimbali ili kuwajengea vijana uwezo wa
kujitambua na kujiwezesha wao wenyewe bila kuwa tegemezi au kuonekana kama ni
mzigo kwa taifa.
Ndugu Wanahabari,Kama sehemu ya kupigania ushiriki na ushirikishwaji
wa vijana kwenye kufanya maamuzi ya mustakabali wao na wataifa, mtakumbuka
mwaka 2010 kabla ya kuelekea uchaguzi
mkuu TYVA iliandaa AJENDA YA VIJANA ambapo dai la katiba mpya inayojali maslahi
ya vijana lilikuwa mojawapo ya madai ya vijana.
Fursa ya kuandika katiba mpya
ilipopatikana, TYVA bado iliendelea kusukuma ajenda za vijana kwa kutoa maoni
kwa tume kwa mlango wa Asasi za Kirai baada ya kukusanya maoni hayo kutoka kwa
vijana mikoani.
Noamba pia kuwajulisha ya kuwa tangu Februari 2011
mpaka Disemba 2012 TYVA imeshiriki michakato yote ya kuandaa katiba mpya ikiwa
ni pamoja kukusanya maoni ya vijana kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajili
ya kuandika katiba Mpya. Tuliwasilisha maoni ya vijana mbele ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba tarehe 9 Januari 2013 katika ukumbi wa Karimjee.
Tuliunda baraza la Katiba la TYVA tarehe 17 Agosti
2013 na kuwasilisha maoni ya kuboresha rasimu ya kwanza ya Katiba Mpya tarehe
30 Agosti 2013.
Ndugu Wanahabari,Kwa hatua ya sasa TYVA inatoa pongezi kwa Tume ya Mabadiliko ya kwa kuweza kutoa rasimu ya pili yenye
marekebisho kadhaa ya maoni ya wananchi ukilinganisha na rasimu ya kwanza.
Ni jambo lililo wazi kuwa rasimu ya
pili imeweza kuongeza vipengele kadhaa muhimu, mfano ni ibara zinazowapa wananchi mamlaka ya moja kwa moja ya kuwawajibisha viongozi wao, kuweka miiko ya
uongozi, Tunu za taifa na utoaji wa huduma za kijamii kwa kila mtanzania kama
haki za msingi, Mfumo wa serekali tatu nakadhalika.
Lakini kwa upande mwingine, bado
kuna ibara hazijaelezewa kwa mapana i, mfano ni ibara ya 44 inayotulenga moja
kwa moja sisi Vijana, Ibara hii imeeelezewa kwa ujumla sana bila kunyambua haki
za msingi na wajibu wa vijana kama inavyotakiwa ikilinganishwa na ibara zingine
katika rasimu hii ya katiba zinazogusa makundi mengine kama ya watoto(43),
wanawake (47) na ya wazee (48).
Ni kwasasababu hii basi TYVA
tunashaui makundi yote ya uwakilishi
kutoka asasi za kiraiya, wabunge na hasa wabunge vijana kulisemea swala
hili na hasa Ibara ya 44 iweze kumwelezea kijana kwa mapana yake katika hali ya
kutatua mazingira magumu vijana wanayopitia ya ukosefu wa ajira, huduma rafiki
za afya kwa vijana, elimu, ukosefu wa mitaji na maeneo ya kufanyia biashara,pia
uongozi na diplomasia.
TUME YA
TAIFA YA UCHAGUZI NEC
Kwa kuwa sheria ya mabadiliko ya
katiba inabainisha kuwa kura ya maoni ya
katiba mpya itapigwa kwa kutumia dafatari la kudumu la mpiga kura, TYVA inatoa
wito kwa tume ya Uchaguz NEC kutoa ratiba ya maboresho ya daftrai hilo mapema
iwezekananyo ili kuepusha malalamiko hasa itakapotokea kuwa zoezi hilo
litafanyika karibu sana na muda wa kura ya maoni ya katiba.
Ni muhimu kutoa muda wa kutosha kwa
zoezi hili kwani NEC haijaboresha daftari hili tangu uchaguzi mkuu wa 2010 na
hivyo kupelekea mamilioni ya watanzania hususani vijana ambao walifikisha umri
wa miaka 18 tangu 2011.
Ni muhimu NEC ikatambuau si chini
ya wiki sita kufanya zoezi hili tofauti na wiki tatu kama ilivyokuwa huko nyuma
kwani pia mabaoresho haya ndio yatabeba picha ya wapiga kura wa uchaguzi mkuu
2015.
Ni matumaini ya TYVA kuona bunge la
katiba kupitiia kwa wajumbe waliopata bahati ya kutuwakilisha vijana tulio
asilimia 65 kati ya idadi ya watanzania wote, hivyo basi tunashauri wajumbe watumie
busara zao kujadili kwa kina ibara hii yenye Majumuisho na kijana azungumziwe
kwa mapana yake katika swala la Haki na Wajibu tofauti na ilivyo sasa. Pia
tunawakumbushi wajumbe wakumbuke bado Vijana wa Tanzania tunakumbana na changamoto
za kutokuwapo na ajira zinazokidhi soko la wahitimu wa kila mwaka katika vyuo
mbalimbali,
BARAZA HURU LA VIJANA
Hiki kitakuwa ni chombo imara sana katika kutunga,
kurekebisha na hata kulishauri bunge katika sera rafiki kwa vijana na Taifa
zima,
Mwisho kabisa sisi vijana kupitia
TYVA tunafahamu changamoto nyingi taifa linazopitia kama vile uongozi mbovu, ukosefu wa ajira, afya, elimu,maji safi na
salama, Rushwa iliyokidhiri,Tatizo la umeme, n.k) kwa upande mwingine
changamoto hizi huathiri sana maendeleo ya vijana na wananchi kwa ujumla kutokana na matatizo ya kimfumo wa
kiutawala tulionao, hivyo upatikanaji wa katiba mpya itakuwa ni mwanzo wa
kubadili mfumo huu na hatimaye kutatua changamoto hizi za sasa na zijazo.
Mwisho kabisa, tunatoa shime kwa
wananchi, bila kujali tofauti zao, kuendelea kushiriki katika mchakato wa
katiba hasa itakapofika wakati wa kura ya maoni ili tupate katiba inayokidhi
matakwa ya wananchi wote kwa ujumla wao.
Imetolewa na:
Elly Ahimidiwe Imbyandumi
Mwenyekiti
(Taifa)- TYVA.
February 4,
2014.
Mwenyekiti
Taifa wa Tanzania Youth Vision Association (TYVA) Elly Imbyandumi,(kushoto) akizungumza na waandishi
Dar es salaam jana kuhusu Bunge Maalumu la Katiba,Wajumbe waweke Maslahi ya
Taifa mbele na Kuzingatia Ustawi wa Vijana.Mwengine ni Ofisa Habari Idara ya
Habari Maelezo,Eliphace Marwa.
No comments:
Post a Comment