Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said akizungumza na Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi kutoka
mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara walio katika mafunzo
ya siku 16 leo mjini Morogoro. Kulia Bw. Mhidini Mtindo, Mtakwimu Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya watu wenye uwezo wa kufanya Kazi kutoka
mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara wakiwa kwenye mafunzo
ya siku mjini Morogoro.
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said akiwa katika picha ya pamoja na Wadadisi na Wahariri kutoka
mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara walio katika mafunzo
ya siku 16 leo mjini Morogoro.
Na. Veronica Kazimoto
na Aron Msigwa – Morogoro.
Wadadisi na Wahariri wa
madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi mwaka 2014 wametakiwa kuzingatia maadili na
weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuepuka kuliletea taifa hasara kwa kutoa takwimu zisizosahihi.
Kauli hiyo imetolewa
leo mjini Morogoro na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said wakati
akizungumza na Wadadisi na Wahariri wa madodoso yaUtafiti wa Watu wenye uwezo wa kufanya kazi kutoka
mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara walio katika mafunzo
ya siku 16 mjini Morogoro.
Amesema ili majibu ya takwimu zinazokusanywa yawe
sahihi ni lazima wataalam hao wazingatie kanuni na taratibu zilizowekwa katika
kupata uhalisia wa taarifa za watu za eneo husika badala ya kutoa takwimu
zisizo sahihi.
“Tunachotegemea kutoka
kwenu ni kwamba mtakayojifunza na kuyafanya kwa vitendo hapa mtakwenda kuyafanyia kazi na kutuletea takwimu
sahihi na sio za kupika mtaani, na kuepuka kuzungumza na watu wachache wa
kikundi Fulani kuwakilisha maeneo yote” Amesisitiza.
Amesema kuwa yapo mambo
mengi ya kuzingatia ambayo wao kama wadadidisi na wahariri wanapaswa kuyafuatilia
wakati wa ukusanyaji wa takwimu hizo ikiwemo idadi ya watu wenye umri wa kwenda
shule ambao bado wako nyumbani ili
kuisaidia serikali kupanga mipango ya maendeleo.
Ameongeza kuwa
ukusanyaji wa takwimu hizo ni muhimu kwa sababu zinaondoa utata katika
kushughulikia changamoto mbalimbali katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwepo wa
usahihi wa taarifa kuhusu makundi ya watu na kazi zao, kipato,masomo, uwezo wa
kufanya kazi na utegemezi na kuondoa
tatizo la baadhi ya taasisi kutumia takwimu zisizo sahihi kujipatia fedha
isivyo halali kwa mambo yasiyokuwepo.
Akitoa ufafanuzi wa
takwimu zilizopo nchini kutokana na matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka
2012 Bi. Hajjat amesema kuwa kiwango cha ongezeko la idadi ya watu kutoka sensa
ya mwaka 2002 mpaka 2012 ni asilimia 2.7 kwa maana ya ongezeko la watu milioni
10 ndani ya miaka 10 na kufafanua kuwa ni sawa na ongezeko la watu milioni 1 kila
mwaka ni kubwa ikilinganishwa na hali ya uchumi uliopo.
Kuhusu mikoa ambayo
wawakilishi wake wako katika mafuzo amesema kuwa mkoa wa Morogoro idadi ya watu imeongezeka kwa
asilimia 2.4, mkoa wa Pwani asilimia
2.2, Dar es salaam 5.6 ongezeko ambalo ni kubwa sana.
“Hii ni changamoto
kubwa sana kwa mkoa wa Dar es salaam na ipo haja ya kuchukua hatua kwa sababu
kila kilometa moja ya mraba wanaishi watu 3133 hata sehemu ya kumwaga taka na
sehemu ya kupitisha maji inakuwa tatizo kutokana na msongamano wa watu’’ amesisitiza.
Aidha katika mkoa wa mkoa
wa Lindi idadi ya watu imeongezeka kwa asilimia 0.9, Mtwara ikifikia asilimia
1.2 na kuongeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa idadi hiyo kuongezeka zaidi kutokana
na ugunduzi wa gesi na mafuta katika mkoa
wa Mtwara ongezeko la watu katika mkoa huo litakuwa kubwa kutokana na uwekezaji
mkubwa katika mkoa huo.
No comments:
Post a Comment