Mbunge wa Rungwe Mashariki na Waziri asiye na Wizara Maalum Profesa
Mark Mwandosya akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu
Godfrey Zambi kwenye uwanja wa Ndege wa Songwe tayari kwa mapokezi ya
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
aliyewasili mkoani Mbeya kwa ajili ya kilele cha sherehe za miaka 37 ya
kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambazo kitaifa zinafanyika mkoani
Mbeya.
:Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo
wakati akizungumza na Mbunge wa Kyela na Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison
Mwakyembe muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete kwenye uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akipungia wananchi wa Mbeya mara tu alipowasili
kwenye uwanja wa kimataifa wa Songwe tayari kwa kilele cha sherehe za
miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM zitakazofanyika kitaifa mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Kikwete akisalimiana na Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip Mangula mara baada ya kuwasili
mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Mbeya Mjini Ndugu Ephraim Mwaitenda kwenye uwanja wa Ndege wa kimataifa
wa Songwe mara baada ya kuwasili kwa ajili ya sherere za miaka 37 ya
kuzaliwa kwa CCM zinazofanyika Kitaifa.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip Mangula akizungumza na
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro mara baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya tayari kumpokea Mwenyekiti wa
CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho
Kikwete.(PICHA NA ADAM MZEE).
No comments:
Post a Comment