Mheshimwa Dkt.Abdulla
Juma Abdulla Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki amehitimisha ziara
yake ya Siku sita kitika Wilaya
zinazotekeleza miradi ya Utunzaji wa Mazingira na Maendeleo endelevu ya
Ziwa Viktoria (LVEMP II ) pamoja na mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira
(LVWATSAN) leo tarehe 8 Februari, 2014.
Kabla ya
kuhitimisha ziara hiyo Mheshimiwa Dkt. Abdalla alitaka kujua maendeleo ya Kituo
cha utafutaji na Uokoaji katika Ziwa
Viktoria kilichopo njini Mwanza na hivyo alitembelea ofisi za Bandari ya Mwanza
kuzungumza na watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Akitoa taarifa
yake kwa mheshimiwa Waziri Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Ndugu Japheti Loisimaye alisema kuwa Bandari ya
Mwanza inahudumia Nchi za Uganda na Kenya na sasa inahudumia pia Sudan ya
Kusini.
Alieleza kuwa
katika ziwa victoria lina visiwa 60 , meli 50 zenye ukubwa wa tani 50 na zaidi. Meli
39 kati ya hizo ziko katika hali nzuri na zinafanya kazi, Meli 11 zimesimamishwa kwa sababu ya kiufundi
na kiusalama. Aliendelea kusema kuwa katika jitihada ya kuboresha uratibu wa
uokoaji na utafutaji pale inapotokea ajali za majini Baraza la Mawaziri wa
Sekta ya Uchukuzi Mawasiliano na Hali ya Hewa
wa Afrika Mashariki katika kikao chao cha tarehe 19-23 Januari 2009
waliidhinisha kujengwa kwa Kituo cha utafutaji na Uokoaji (MRCC) katika jiji la Mwanza. SUMATRA
ilitenga eneo la ofisi za muda katika jengo la
NSSF jijini Mwanza wakati jitihada zikifanywa kupata eneo la kudumu la
ujenga kituo hicho kitakachokuwa chini ya Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria
(Lake Victoria Basin Commission – LVBC) ambayo ni taasisi ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Aliendelea
kusema kuwa kiwanja tayari kimepatikana kwa ajili ya kujenga kituo hicho na
hati ya kiwanja hicho tayari imetolewa. Mheshimiwa Naibu Dkt. Abdulla alipata
nafasi ya kutembelea kiwanja hicho ambacho kipo karibu na bandari ya Mwanza
North. Aidha aliwapongeza SUMATRA kwa hatua iliyofikiwa na
kuwahimiza kuwa wanunue vifaa kama vile radio calls ma vifaa vya ofisi wakati
jududi za kutafuta pesa za ujenzi wa kituo hicho unaendelea.
Aliendelea kusema kuwa Watumishi wamejipanga
vizuri kutoa huduma ila tatizo ni Reli kutoka Dar es Salaam kuja Mwanza
kutokufanya kazi, hivyo kupungua sana kwa mizigo. Mizigo inayosafirishwa kwa
wingi kwa sasa ni unga wa Bakhressa unaosafirishwa kwa maroli kutoka Dar es
Salaam na baadaye kusafirishwa kwa meli kwenda Uganda na Sudan ya Kusini. Aliendelea
kusema kuwa kuna wafanyabiashara wengi kutoka Uganda ambao wanatumia Bandari ya
Mwanza na hivyo hulazimika kupakia mizigo yao Mwanza hadi bandari ya Kemondo
Kagera na kisha kupakia mizigo hiyo kwenye maroli kuelekea Uganda na Sudani ya
Kusini.
Naye Capt
Mkongoki alieleza kuwa Mwaka 1999 kulikuwa na meli iliyokuwa inakwenda Portbell
Uganda ila ilionekana inapata abiria wachache kwa kwenda Portbell Uganda kwani ilikuwa na uwezo wa kubeba
abiria 1200 lakini ilikuwa ikipata abiria kati ya 200-300. Kwa sasa imeonekana
kuna mahitaji makubwa ya meli kwenda Portbell Uganda, Danida italeta meli mpya
mwaka kesho (2015) na meli hiyo inategemea kuanza kazi mwaka 2016. Hii ni kwa
ajili ya kurahisha usafiri na usafirishaji katika nchi za Afrika Mashariki.
Aidha alieleza
kuwa kupitia Mpango wa matokeo Makubwa sasa (BRN) Serikali imetoa shilingi
bilioni tano (5) kwa ajili ya kuboresha
Bandari ya Mwanza , hata hivyo Serikali inatakiwa kuweka nguvu kubwa katika
kujenga reli na pia kuweka mkakati wa kulima zaidi badala ya kuzuia chakula
kuuzwa nje ya nchi.
Naye Mheshimwa Dkt.Abdulla
aliongeza kuwa mojawapo ya vipaumbele
vya Tanzania ni kuwa ghala la chakula kwa nchi za Afrika Mashariki na hivyo
tayari serikali imeweka na inaendelea kutekeleza mpango wa Kilimo kwanza ili kuhakikisha
Tanzania inazalisha zaidi mazao ya kilimo na kuuza katika nchi za Afrika
Mashariki.
Communications Expert
Ministry of East African Cooperation (MEAC)
P. O. Box 9280,
Dar es Salaam
TANZANIA
skype: faraja101
+255 754 271 750
Ministry of East African Cooperation (MEAC)
P. O. Box 9280,
Dar es Salaam
TANZANIA
skype: faraja101
+255 754 271 750
Naibu
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Abdulla Juma
Saadalla akioneshwa kiwanja kitakachotumika kujenga kituo cha utafutaji
na uokoaji katika ziwa Victorai (MRCC) njini Mwanza
Mr Faraja Mgwabati
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Abdulla Juma Saadalla akitembelea Bandari ya Mwanza.
No comments:
Post a Comment