Mkurugenzi wa Msama Promotions akimkabidhi Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa Islamic Orphans,Halima Mpeta sehemu ya misaada hiyo.
Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama akimkabidhi mtoto Heid Din wa Kituo cha Watoto Yatima cha (TOVUCHIDO) mafuta ya kupaka mwilini.
Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama akimkabidhi fedha tasilimu mfanyakazi wa Kituo cha (TOVUCHIDO) Honoratha Michaes.
Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama akimkabidhi hundi Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa Islamic Orphans,Halima Mpeta sehemu ya misaada hiyo.
Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama akiwakabidhi watoto wa
Kituo cha Yatima cha Malaika.
Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama akiwakabidhi hundi watoto wa
Kituo cha Yatima cha Malaika.
Msama akabidhi misaada kwa vituo vitatu.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Msama Promotions waandaaji wa
Matamasha ya Kirimasi na Pasaka jana ilikabidhi misaada mbalimbali kwa
vituo vitatu vya jijini Dar es Salaam, ikitimiza ahadi ya kuisaidia jamii kabla
ya Tamasha la mwaka huu linalotarajia kuanza Aprili 20 hapa nchini.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama misaada hiyo iliyogharimu
shilingi milioni 7 imekabidhiwa katika vituo vya TUVUCHIDO cha Temeke Maganga,
Malaika Kids cha Mwananyamala na kituo cha Yatima cha Mwandaliwa.
Msama
alisema katika sehemu ya msaada huo pesa taslim shilingi milioni 2.9 ni ada kwa
wanafunzi na nyingine ni kwa vifaa mbalimbali yakiwemo madaftari, sabuni za
mche, unga, mafuta ya kupaka na sukari.
Aidha
Msama alisema misaada hiyo imetokana na mfuko wa Tamasha la Pasaka kama
ilivyokuwa kwenye Tamasha la Krismasi ambalo walikabidhi misaada ya shilingi
milioni 7.
Mkurugenzi
wa TUVICHIDO, Honarata Michael alimpongeza Msama kwa kuwajali watoto na jamii
kwa ujumla.
Naye
Mkurugenzi wa kituo cha Mwandaliwa, Halima Mpeta alisema anamshukuru Msama kwa
kujali jamii kwani katika kituo chake si mara ya kwanza kukisaidia na amezidi
kumuomba aendelee na moyo wa kukisaidia kituo chake na vingene vyenye mahitaji.
No comments:
Post a Comment