Na Mwandishi Wetu
WAKATI
Tamasha la Pasaka kinatarajia kufanyika mwaka huu kwenye mikoa mbalimbali hapa
nchini, mashabiki wa tamasha hilo ndio watachagua mikoa itakayofanyika.
Mfumo
huo utasaidia mashabiki wa mikoani kuteua mikoa yao ifikiwe na tamasha hilo la
kumuimbia na Kumtukuza Mungu kupitia nyimbo na mapambio kupitia nyimbo
mbalimbali.
Wakati
taratibu za maandalizi zikiendelea, Kampuni ya Msama Promotions ambao ndio
waandaaji wa tamasha hilo hivi sasa wanasubiri kibali kutoka Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA).
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama bado tunasubiri Basata
watakabidhi kibali cha kufanikisha tamasha hilo ambalo mikoa sita imeonesha.
Msama
alisema tamasha la mwaka huu wamejipanga kusikiliza mikoa mingi zaidi kwa
sababu inaonekana mikoa mingi ina kiu ya kupata neno la Mungu kupitia waimbaji
mbalimba wa Tanzania na nje.
Aidha
Msama alisema wako kwenye mchakato wa kuandaa mfum ambao utafanikisha mikoa
kujipigia kura.
Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka na
Krismasi, Kampuni ya Msama Promotions imewaomba wadau wenye nia ya kufanikisha
maendeleo ya matamasha hayo kuwasaidia katika muendelezo wa matamasha
yanayoandaliwa na kampuni hiyo, Aprili
mwaka huu kampuni hiyo iko mbioni kuandaa Tamasha la Pasaka.
Kutokana na hali hiyo, wadau mbalimbali ambao
wamepata kutoa ahadi za namba mbalimbali katika matamasha hayo wameombwa
kutekeleza ahadi zao ili zitumike katika malengo yaliyokusudiwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la
Pasaka, Alex Msama alisema wadau mbalimbali wa muziki wa Injili, wakiwemo
baadhi ya viongozi wamekuwa wakitoa ahadi ambazo utekelezaji wake umekuwa
mgumu.
“Wapo baadhi ya watu wanakuja katika matamasha
yetu, wanatoa ahadi nzito hasa za fedha, lakini tamasha likishamalizika
wanashindwa kutekeleza ahadi zao na ndiyo huwaoni tena, tunashukuru wapo
wengine huwa wepesi kutimiza walichoahidi.
“Huwa haya matamasha tunayaandaa kwa malengo
maalum, ukitaja ahadi yako huwa tunaipa thamani kubwa na ukishindwa kuitimiza
unatuangusha na hilo ndilo linatuharibia sana mipango yetu,” alisema Msama
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi.
Aliwaomba baadhi ya viongozi na wadau wengine
ambao wamepata kutoa ahadi mbalimbali kwenye Tamasha la Pasaka kuhakikisha
wanatekeleza ahadi zao kama walivyozitoa na kusisitiza kuwa hakuna sababu ya
kuwataja majina kwani wenyewe wanajitambua.
“Tunaamini pengine wana mambo mengine ndiyo
sababu tumeandika barua kuwakumbusha wakati huu tukielekea katika maandalizi ya
Tamasha la Pasaka,” alisema.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Msama Promotions ambayo ndio waandaaji wa
Tamasha la Pasaka na Krismasi inalifikisha suala la mgeni rasmi wa Tamasha la
mwaka huu linalotarajia kuanza Aprili 20 katika mikoa sita hapa nchini.
Pamoja
na kuwa katika mipangilio hiyo, kampuni hiyo inasubiri taratibu za upatikanaji
wa kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili kufanikisha tamasha
hilo.
“Tunasubiri
taratibu za Basata ili kufanikisha upatikanaji wa kibali kutoka Basata ili
tufanye tamasha katika mfumo wa kisasa zaidi,” alisema Mkurugenzi wa Msama
Promotions, Alex Msama.
Kwa
mujibu wa Msama wakati wanasubiri kibali kutoka Basata wanajipanga
kuwashirikisha mashabiki wa muziki wa Injili hapa nchini kuteua mgeni rasmi
katika tamasha hilo.
Aidha
Msama alisema tamasha la mwaka huu litakuwa ni la kisasa zaidi kwa sababu
litashirikisha mashabiki na wadau kuteua mgeni rasmi na maendeleo mengine
katika tamasha hilo.
Msama
alisema watakachoamua mashabiki ndicho watakachokitekeleza hasa kwenye suala la
mgeni rasmi.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Msama Promotions, imeingiza sokoni albamu ya Msaada wangu wa Karibu yenye
nyimbo nane iliyoandaliwa na mwimbaji Grace Mwikwabe.
Kwa
mujibu wa mwimbaji wa albam hiyo,
Mwikwabe Msama Promotions imefanikisha Audio na Video ya albamu hiyo ya
kwanza katika tasnia hiyo ya muziki wa Injili.
Mwikwabe
alitoa shukrani kwa Mungu ambaye amefanikisha maendeleo yake pia anamshukuru
Msama kwa msaada aliompa katika kufanikisha kazi zake.
Aidha
Mwikwabe alizitaja nyimbo zilizopo kwenye albam hiyo ni pamoja na Msaada wa
Karibu, Mbali sana nimetoka, Watu wote waokoke, Eeh baba Mungu, Waringa na
Kujisifu, Sifa ni kwako bwana, Tumaini
lako bado lipo na Mwambie Yesu.
Mwikwabe
alitoa wito kwa waumini mbalimbali kujitokeza kuinunua albam hiyo ambayo
imegusa nyanja zote mbalimbali.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Msama Promotions iko katika mchakato
wa kuandaa Tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza Aprili mwaka huu huku mikoa
sita ikihitaji kufanyika kwa tamasha hilo.
Tamasha la mwaka huu linalosubiri taratibu za
kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mwaka huu limejipanga kuja
katika mtindo mwingine ambao ni wa kisasa zaidi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions,
Alex Msama mipangilio hiyo ni pamoja na kuwashirikisha mashabiki wa muziki huo
ili kuchagua baadhi ya taratibu ambazo ni muhimu na wao wakashirikishwa kwa
sababu tamasha hilo ni lao.
Msama alisema tamasha la mwaka huu mpango wake
ni kuendeleza mikakati ya ujenzi wa kituo cha wenye uhitaji maalum
kitakachojengwa eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambacho ni
‘Jakaya Mrisho Kikwete rafiki wa walemavu’.
Aidha Msama alisema ujenzi wa kituo hicho
utafanikishwa pia kupitia Tamasha la Pasaka la mwaka huu ambalo limejipanga
kufanikisha ujenzi huo kuptia tamasha la
mwaka huu.
“Tunatoa wito kwa wadau kujipanga kwa ajili ya
kufanikisha mipangilio ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitafanikishwa kupitia
wadau mbalimbali ambao michango yao ndio itafanikisha maendeleo hayo,” alisema
Msama.
Msama alisema kituo hicho kitawahusu walemavu, wajane, wanaoishi katika mazingira
hatarishi na wenye uhitaji maalum.
Msama alisema kamati yake bado itaendeleza
mipangilio yake ya kufanya tamasha hilo kwa kushirikiana na waimbaji wa
Kimataifa kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, tamasha la mwaka jana mwimbaji
Rebecca Malope ni mmoja wa waimbaji waliolinogesha tamasha hilo sambamba na
waimbaji wengine kama Rose Muhando, Upendo Nkone (Tanzania) na wengineo.
Baadhi ya mikoa ambayo iliyoonesha kuhitaji
kufanyika kwa tamasha hilo ni pamoja na Morogoro, Iringa, Mbeya, Dodoma,
Shinyanga na Mwanza.
No comments:
Post a Comment