KAOHSIUNG NA JESHI LA POLISI KWA WAHITIMU WATARAJIWA WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014
Katika
mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi linatarajia kuajiri wahitimu wa
kidato cha sita mwaka 2014 na kidato cha nne mwaka 2013. Ili kutekeleza
azma hii tumeweka fomu kwenye tovuti ambayo wahitimu watarajiwa wa
kidato cha sita wa mwaka 2014 watajaza kabla ya kufanya mitihani yao ya
kumaliza kidato cha sita.
Baada ya
kujazwa kikamilifu wakabidhi fomu kwa wakuu wa shule ambao watazirejeshe
kwa Makamada wa Polisi wa mikoa kabla ya tarehe 17.03.2014. Wahitimu wa
kidato cha nne wasijaze fomu hizi walishajaza kupitia “selform”
walizojaza walipokuwa shuleni.
MASHARTI KWA MWOMBAJI:
1.Mwombaji
anatakiwa ajaze fomu hii kikamilifu na abandike picha yake “Passport
Size” kwenye fomu kisha akabidhi kwa Mkuu wa Shule kwa hatua zaidi.
2.Kila mwombaji aandike namba ya simu kwa usahihi na anuani yake ya kudumu ambayo itatumika wakati wa kuitwa kwenye usaili.
3.Pakua:Fomu ya Chaguo hapa...
Imetolewa na:
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.
Chanzo: Jeshi la Polisi Tanzania
No comments:
Post a Comment