Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Kebwe Kebwe
amewataka viongozi wa halmashauri kushirikiana na waganga wakuu
kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinavyotolewa na Serikali kupitia Bohara
Kuu ya Dawa MSD vinatumika ipasavyo.
Dkt. Kebwe alisema hayo jana wilayani Masasi Mkoani Mtwara katika ziara
ya kwanza toka uteuzi wake kutoka kwa Rais Kikwete wakati akiwa na
kamati ya kudumu ya Bunge huduma za jamii kukagua taratibu za
usambazaji dawa vituo na hospitali za Serikali.
Katika ziara hiyo amezitaka Hospitali za Serikali kutumia vyanzo vingine
vya mapato ili kuweza kununua dawa na vifaa tiba katika kuongezea
matumizi mbalimbali na bajeti ya Serikali.
“ni muhimu kuelewa kuwa hospitali inavyanzo vingi vya mapato wakati
umefika sasa kutumia fursa hizo katika kuhakikisha mapato yanayotokana
na vyanzo vya hospitali yanatumika pia katika kuongeza ununuaji dawa na
vifaa tiba ili kuipa uwezo Serikali na jamii kufikia huduma
ipasavyo”alisema
Naye Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge huduma za jamii Magreth
Sita alisema ni muhimu suala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kupewa
kipaumbele cha hali ya juu kutokana na kuwa ndio msingi wa huduma bora
za afya kwa jamii.
Alisema kutokana na ufanisi mkubwa uliopo katika upatikanaji dawa
hospitalini na vituo vya afya baada ya mfumo wa ufikishaji dawa moja kwa
moja hadi vituoni (DD) unaofanywa na MSD ni vizuri Serikali kutambua
kuwa ufanikishaji wa hatua hiyo unahitaji uwezeshi hasa wa fedha za
bajeti kufika kwa wakati.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya wadhamini MSD Dkt Ahmed Hingola
alisema endapo Serikali itadhiti na kuhakiki dawa chache zilizopo ili
kutekeleza mahitaji ni wazi lawama za wananchi kwa bohari ya dawa
zitakwisha.
“MSD kazi yake kubwa ni upelekaji wa dawa huku usimamizi wa matumizi
katika kutumika kama ilivyokusudiwa ikiwa bado ni changamoto hasa katika
sehemu husika hivyo MSD imeanza harakati za uwekaji wa nembo dawa za
Serikali (GoT) ili kudhibiti dawa hizo zisiweze kupita njia za
panya”alisema
No comments:
Post a Comment