Na Anna Nkinda –
Maelezo
Umoja wa
Wanawake wa Tanzania (UWT) umempongeza Mhe.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba linalotarajia
kuanza leo Mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari na kusainiwa na
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Eva Mwingizi ilisema uteuzi wa Rais umezingatia
umri, weledi, uzoefu na uwakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii.
Mwingizi alisema uteuzi
huo umeangalia asilimia 50 ya uwakilishi wa wajumbe 201 hii ikiwa ni wanawake
100 na wanaume 101 pia Bunge hilo linajumuisha wabunge wote wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano na wajumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar.
Aidha katibu Mkuu huyo alilitakia
heri Bunge hilo na kuwaomba wajumbe waliochaguliwa kutambua kuwa wamepewa
dhamana kubwa ya kuzingatia maoni ya wananchi ya kutengeneza katiba ya Tanzania
yenye kulinda, kutetea na kusimamia
maslahi ya Taifa kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.
No comments:
Post a Comment