Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni
mpaka kati ya Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani
Buhigwe mkoani Kigoma leo Alhamisi, Aprili 10, 2014. Kinana yupo katika
ziara ya siku tano mkoani humo ya kukagua uhai wa Chama na kusikiliza
kero za wananchi mkoani humo. Moja ya kero kwenye mpaka huo
unaokutanisha vijiji vya Kibande (Tanzania) na Murambi(Burundi) ni
Watanzania kulazimika kukumbana na adha ya kuvuka mto huo kwenda kufanya
biashara na kununua mahitaji kwenye soko lililopo upande wa Burundi.
Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
Kinana
akitazama mpaka huo na namna wananchi walivyokuwa wakivuka na wengine
kuvushwa kwenye mto wa Malagarasi wakitoka Burundi kuingia Tanzania
Eneo
la soko la Murambi, Burundi ambako Watanzania hulazimika kwenda
kufanyabiashara na kupata mahitaji huko kutokana na upande wa nchi yao
kutokuwa na soko ikiwemo la mifugo lililokuwepo zamani na sasa halipo
kutokana na kufungwa kwa sababu zisizojulikana, ambaopo Kinana alihoji
kwa nini lisiwepo soko upande wa Tanzania ili kuondoa kero ya watu
kuvuka mto kila siku kwenda ng'ambo.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa pembezoni mwa mto
Malagarasi, mpakani mwa Tanzania na Burundi wakati wa ziara hiyo.
Juu ya maelezo haya ni wananchi wakivuka mto Malagarasi kutoka upande wa Burundi kuingia Tanzania
Baadhi
ya wananchi wakiwa wameingia Tanzania baada ya kuvuka mto huo kwa
taabu, baadhi yao wameomba serikali za nchi hizo kujenga daraja kwenye
mto huo kurahisisha uvukaji
Wananchi
wa Kijiji cha Buhigwe wakimlaki Kinana alipowasili kwenye Ofisi ya CCM
Kata ya Buhigwe, kuzungumza na Kamati ya Siasa ya CCM wilayani humo, leo
Kinana
akizungumza na wananchi hao baada ya kumaliza kuzungumza na Kamati hiyo
ya siasa. Kulia ni Mbunge wa Buhingwe maarufu kwa jina la Obama
Katibu Mkuu wa CCm Abdulrahman Kinana akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Buhigwe wakati wa mkutano huo
Katibu
wa NEC, Itkadi na Uenezi, Nape Nnauye akicharaza ngoma, Kikundi cha
Kerebuka kilipotumbuiza kwenye mkutano wa Kinana na wananchi wa Buhigwe
Msanii
wa kikundi hicho cha Kerebuka kutoka Burundi akionyesha umahiri ake wa
kucheza ngoma ya taifa ya nchi hiyo kwenye mkutano huo wa Kinana
uliofanyika Buhigwe
Nape
akiwa amezungukwa na watoto wa Kijiji cha Kibande, wakati akifanya kazi
zake kwenye kompyuta pambeni mwa mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja
vya Kijiji hicho kata ya Buhigwe
Msafara
wa Kinana ukiwasili kwenye mpaka wa Tanzania na Burundi uliopo Kata ya
Munanila, Manyovu wilayani Buhigwe mkaoni Kigoma
Baadhi ya matangazo kwenye mpaka huo
Kinana na msafara wake wakitazama eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi kwenye Kijiji cha Munanila, Tarafa ya manyovu
Vijana
wa Kijiji cha Munanila, tarafa ya Manyovu wilayani Buhigwe
wakimuonyesha Kinana na msafara wake, uhodari wao wa kucheza ngoma ya
Kasimbo ya Kiha, kwenye mkutano uliofanyika Munanila
Kinana akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Munanila wilayani Buhigwe.
Kinana
akiwapungia mikono wananchi baada ya kumfurahisha kwa mapokezi yao,
Kijiji cha Munanila alipoowasili kwa ajili ya mkutano wa hadhara
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa na Kinana, Munanila, Buhigwe
Katibu
Mkuu wa CCm, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Kijiji cha Munanila, Tarafa ya Manyovu wilayani
Buhigwe mkoani Kigoma leo jioni
Wananchi wa Munanila wakimshangilia Kinana alipohutubia kwenye mkutano huo. (Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog)
No comments:
Post a Comment