Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.) akisalimiana na Gavana wa Jimbo la Maryland la nchini Marekani,
Mhe. Martin O'Malley walipokutana jijini Washington D.C kwa mazungumzo
kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Jimbo hilo na Tanzania
katika masuala ya uchumi, jamii na siasa. Mhe. Membe alipata fursa ya
kukutana na Gavana huyo alipokuwa mjini humo kwa ajili ya kumwakilisha
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwenye upokeaji Tuzo ya Kiongozi mwenye Mchango Mkubwa zaidi katika
Maendeleo ya Bara la Afrika kwa Mwaka 2013. |
No comments:
Post a Comment