Na Anna Nkinda- Maelezo,
Lindi
Wakazi wa
kata ya Msinjahili wilayani Lindi wametakiwa kutoogopa kuvuta umeme majumbani
mwao kwa kuhofu kuwa wakifanya hivyo wataonekana ni matajiri kwani matumizi ya
umeme ni ya gharama naafuu ukilinganisha na mafuta ya taa.
Mwito huo umetolea jana
na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) wilaya ya
Lindi mjini wakati akiongea kwa nyakati
tofauti na viongozi wa Halmashauri kuu
ya tawi ya Chama hicho katika matawi
ya Muungano, Jitegemee, Sinde na Mnali
yaliyopo katika kata ya Msinjahili wilaya ya Lindi mjini.
Mama Kikwete ambaye pia
ni Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alisema ili kuboresha maisha ya wananchi Serikali imejitahidi kupitisha
umeme wa gesi katika vijiji vilivyopo katika kata hiyo na
kupunguza gharama ya uvutaji ambazo ni nafuu jambo la muhimu ni kwa wananchi kuutumia.
“Kuwa na umeme nyumbani
kwako na kuutumia ni mwanzo wa maendeleo, hata watoto wako wataweza kuutumia mwanga huo
kwa kujisomea hasa nyakati za usiku na hivyo
kufanya vizuri katika mitihani yao”, alisema Mama Kikwete.
Aidha Mjumbe huyo wa
NEC pia aliwataka viongozi hao
wa Halmashauri kuu ya tawi kuwahimiza watu wanaowaongoza katika maeneo
yao kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kulima chakula cha kutosha jambo ambalo
litawafanya kuwa na chakula cha ziada na hivyo kuepukana na kitendo cha kuomba chakula kwa majirani.
Akizungumzia kuhusu
suala la uongozi Mama Kikwete aliwahimiza wanawake kutoogopa kuomba na kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi katika chaguzi
zijazo ili waweze kupata nafasi ya
kuongoza na hivyo kufika katika ngazi ya maamuzi.
Mama Kikwete
alisisitiza , “Sisi wanawake tunakabiliwa na changamoto nyingi na mtu pekee anayeweza kuziongelea changamoto
zetu kiusahihi ni mwanamke mwenyewe hivyo basi msiogope kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi wakati wa uchaguzi ukifika mkifanya hivyo kutakuwa na
viongozi wengi wanawake ambao wataweza kuwakilisha matatizo na mawazo yetu
katika ngazi za juu za uongozi wa chama na Serikali”.
MNEC huyo alimalizia
kwa kuwahimiza viongozi hao wa Halmashauri kuu ya tawi ya CCM kuishi maisha ya upendo, mshikamano na amani kwani jamii ikiishi
maisha hayo itaweza kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana.
Kwa upande wake katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Lindi Haji
Tajiri aliwataka viongozi hao kuwa waaminifu katika ndoa zao na kuepuka tabia ya kuwa na mpenzi zaidi ya
mmoja (michepuko) kwa kufanya hivyo wataepukana na ugonjwa wa Ukimwi.
“Chama Cha Mapinduzi kinahitaji kuwa na watu wenye afya njema ili
waweze kufanya vizuri kazi za chama nawaomba muwe waaminifu kwa wapenzi wenu
mkifanya hivyo mtaepekana na Ugonjwa wa Ukimwi”, alisema Tajiri.
Katibu huyo wa Jumuia
ya Wazazi mkoa pia aliwaomba kinamama kuiga mfano wa Mama Salma Kikwete ambaye anafanya
kazi kubwa ya kujitoa katika shughuli mbalimbali za kijamii na kutetea haki zao,
wasichana na watoto na kuongeza kwamba
anastahili pongezi kwani yeye ni mama na mlezi wa taifa.
Mjumbe huyo wa NEC
taifa akiwa katika kata ya Msinjahili alifungua mashina ya wakereketwa wa CCM
Jumuia ya wazazi katika tawi namba tatu la
Sinde na namba mbili la Mnali.
No comments:
Post a Comment