Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
wa Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini
mtoto Idd Omar kutoka katika Kijiji cha Madangwa , kata ya Sudi huko Lindi
Vijijini. Mama Salma alifika kijijini hapo kwa ajili ya kupokea mbio za
uzalendo za pikipiki zilizoandaliwa na Umoja wa Vijana, (UVCCM) kitaifa
zikitokea Mkoa wa Mtwara.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya
Madangwa namna ya kushika mfagio ili usiweze kuleta madhara kwa watoto
waliobeba na hata wengine na pia ni njia bora ya kulinda afya zao kwani
wakishika upande unaotumika kufagia wanaweza kupata magonjwa ya kuambukizwa.

Baadhi ya
wasichana na akina mama wakionyesha umahiri wao katika kucheza ngoma za
utamaduni wakati wa sherehe ya makabidhiano ya mbio za pikipiki kutoka mkoani
Mtwara kwenda Mkoa wa Lindi katika Kijiji cha Madangwa.
Mwenyekiti
wa CCM wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Said Sinani (mwenye kofia) akifuatana na
viongozi wenzake wa Chama Cha Mapinduzi na Umoja wa Vijana kwenda kukabidhi
mbio za pikipiki kwa uongozi wa Mkoa wa Lindi kwenye Kijiji cha Madangwa.
No comments:
Post a Comment