Mkuu wa Mkoa
wa Kilimanjaro Ndugu Leonidas Gama akimpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Mama Salma
alikwenda Moshi kuzindua rasmi chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya
shingo ya kizazi kwa wasichana wa umri wa miaka 9 hadi 16.
Mke wa Rais
na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete
akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia watoto, UNICEF, hapa nchini
Dkt. Sudha Sharma, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mandela uliopo
katika eneo la Pasua katika Manispaa ya Moshi kwa kulikofanyika uzinduzi rasmi
ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma na vikundi vya kwaya vilivyokuwa
vikitumbuiza wakati wa sharehe za uzinduzi wa chanjo ya kuzuia saratani ya
shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 16.
Maandamano ya vikundi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro wakipita
mbale ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa chanjo
kwenye uwanja wa Mandela huko Pasua mjini Moshi.

Mamia
ya watu waliohudhuria sharehe za uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya
saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wakifuatilia kwa makini hotuba ya
Mgeni rasmi, Mama Salma Kikwete katika sherehe hiyo.

Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi na wanafunzi waliohudhuria
sherehe za uzinduzi rasmi wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa
wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 16 huko Pasua, Moshi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo
ya kizazi kwa wasichana kwenye sherehe iliyofanyika huko Pasua, Moshi Mjini. Wengine katika picha (kushoto kwenda kulia) ni Ndugu Leonidas
Gama, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Rufaro Chatora, Mwakilishi wa Shirika
la Afya Duniani hapa nchini, Dkt Kebwe Stephen Kebwe, Naibu Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila, Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya
Afya, Mama Salma na wa Kwanza kulia ni Mwakilishin wa Shirika la Kuhudumia
watoto (UNICEF) hapa nchini Dkt. Sudha
Sharma.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiandika taarifa za mtoto Salma Abillah mara baada ya
kupata chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi na baadaye kumkabidhi kadi
yake ambayo anatakiwa kurudi tarehe 28.10.2014 kwa ajili ya kupata chanjo ya
pili.

pili.(PICHA NA JOHN LUKUWI.)
No comments:
Post a Comment