Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa
Macho wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Frank Magupa, wakati alipotembelea maonesho
ya kitabibu yaliyofanyika sambamba na upimaji wa saratani ya shingo ya
kizazi kwa wanawake wa wilayani Bahi.
Mamia ya wananchi wa Bahi wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa
zinatolewa na viongozi wa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa upimaji wa
saratani ya shingo ya kizazi iliyofanyika huko Bahi, Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Kebwe Staphen Kebwe akitoa
salamu hotuba kwa niaba ya wizara ya Afya wakati wa uzinduzi wa upimaji
wa saratani ya shingo ya kizazi huko wilayani Bahi.
Mamia ya wananchi wa Bahi wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa
zinatolewa na viongozi wa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa upimaji wa
saratani ya shingo ya kizazi iliyofanyika huko Bahi, Mkoani Dodoma.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa wilaya
ya Bahi muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi kampeni ya upimaji wa
saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake katika wilaya ya Bahi mkoani
Dodoma.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya
kizazi kwa wanawake wa Wilaya ya Bahi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha vifaa mbalimbali
vinavyotumika na madaktari wakati wa kuwapima wanawake ili kufahamu kama
wana maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi wakati wa uzinduzi wa
kampeni hiyo wilayani Bahi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na wacheza ngoma na wananchi
mbalimbali wa wilaya ya Bahi mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa
saratani ya shingo ya kizazi kwa akinamama.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti Mwakilishi wa Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC1) Bwana Hamis Mwege kwa kazi kubwa ya
kuelimisha umma kuhusu kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya
kizazi kwa wanawake hapa nchini. Vyombo vingine vilivyopata cheti ni
Channel Ten na ITV.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama
Salma Kikwete akiwapungia wanafunzi na wananchi wa Bahi waliohudhuria
sherehe ya uzinduzi wa saratani ya shingo ya kizazi mjini hapo.(PICHA NA JOHN LUKUWI)
No comments:
Post a Comment