Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka
20 (Ngongoro Heroes) imereja nchini leo mchana (Aprili 7 mwaka huu) kutoka Kenya
mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya wenyewe, na itaingia kambini Alhamisi.
Ngorongoro Heroes ambayo imewasili saa 8.25 kwa
ndege ya Kenya Airways ilitoka suluhu na Kenya katika mechi iliyochezwa Uwanja
wa Kanyetta uliopo katika mji wa Machakos.
Kocha John Simkoko amesema benchi lake la ufundi
linafanyika kazi upunguzi uliojitokeza ili wafanye vizuri kwenye mechi ya
marudiano itakayochezwa Aprili 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Iwapo Ngorongoro Heroes itaitoa Kenya, raundi
inayofuata itacheza na Afrika Kusini. Fainali za Afrika kwa vijana chini ya
miaka 20 zitafanyika mwakani nchini Senegal.
PONGEZI KWA TIMU YA WATOTO WA MITAANI
Tunaipongeza
timu ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani kwa kutwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa
Mitaani baada ya jana (Aprili 6 mwaka huu) kuifunga Burundi mabao 3-1 katika
mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Ushindi
kwa timu hiyo ni fahari kwa Tanzania, lakini kubwa ni kwa kituo cha Mwanza
ambacho ndicho kinachoiendesha pamoja na wadhamini na wafadhili walioiwezesha
kushiriki fainali hizo kwa mara ya pili mfululizi.
Vilevile
ushindi huo unatoa changamoto kubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kuwa watoto wa
mitaani ni sehemu tu ya vipaji vilivyotapaa nchini, hivyo iliyopo ni kuvisaka
na kuvibaini vipaji hivyo kwa ajili ya ustawi wa mchezo huo nchini.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tutaendelea kushirikiana na kituo hicho cha
Mwanza, na vingine vyote ambavyo vinajishughulisha na mchezo huu, lengo likiwa
ni kuundeleza na hata kutoa ajira kwa vijana hapo baadaye kupitia mpira wa
miguu.
Timu hiyo
inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment