Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka
20 (Ngongoro Heroes) inarejea nchini leo (Aprili 7 mwaka huu) kutoka Kenya
ambapo jana (Aprili 6 mwaka huu) ilicheza mechi ya michuano ya Afrika.
Ngorongoro Heroes ambayo itatua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.25 mchana kwa ndege ya Kenya Airways
ilitoka suluhu na wenye Kenya katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kanyetta
uliopo mji wa Machakos.
Timu hizo zitarudiana jijini Dar es Salaam wiki
tatu baadaye ambapo itakayofuzu itacheza raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini.
Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 zitachezwa mwakani nchini
Senegal.
TIMU YA WATOTO WA MITAANI YATWAA UBINGWA WA DUNIA
Timu ya Taifa
ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani
baada ya jana (Aprili 6 mwaka huu) kuilaza Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali
uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Mshambuliaji
Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja
mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa
Fedha wa Uingereza, George Osborne.
Tanzania
ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo
hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0.
Burundi
ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi
ya nusu fainali ya pili.
Timu ya
Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment