Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi
kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga leo, Mei 9, 2014, akiwa katika
ziara ya siku kumi kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM,
kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua na pia
kuimarisha uhai wa chama mkoani Tabora
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape NNauye akizungumza kwenye mkutano huo
Maelfu
ya wananchi wakinyoosha mikono kumshangilia Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara Mei 9, 2014, kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga
Mkuu
wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora Elibariki Kingu, akieleza utekelezaji
wa ilani ya CCM kwenye mkutano huo wa Kinana auliofanyika, Mei 9, 2014
kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine wilayani humo.
Kinana akirudi hotelini kwa miguu baada ya mkutano, pembeni yake ni Nape
KUIMARISHA UHAI WA CHAMA
Kinana akirudi hotelini kwa miguu baada ya mkutano, pembeni yake ni Nape
KUIMARISHA UHAI WA CHAMA
Kinana akizindua Ofisi ya CCM tawi la Igogo, Kata ya Nanga Igunga, mkoani Tabora, leo Mei 9, 2014
Kinana akizungumza baada ya kuzindua Ofisi hiyo ya CCM tawi la Igogo, Kata ya Nanga Igunga. Kulia ni Nape
Kinana akisalimia baadhi ya wazee baada ya kuzindua tawi hilo la CCM
Kinana
akishiriki ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya msingi Mihama, Igunga
mkoani Tabora, Mei 9, 2014. Kushoto ni DC Igunga, Elibariki Kingu
akisaidia kubeba tofali kumpa Katibu Mkuu Kinana.
Kinana
akiwa na bango lenye ujumbe maridhawa, kumkaribisha Kinana,
alipotembelea shamba la alizeti la Vijana wajasiriamali, eneo la
Iborogero, wilayani Igunga mkoani Tabora, Mei 9, 2014, ikiwa ni sehemu
ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika muktadha wa ajira kwa
vijana.
Kinana akikagua shamba hilo la alizeti la Vijana la Iborogelo
Kinana akitazama zao la alizeti alipokagua shamba hilo la alizeti la Vijana la Iborogelo
HADI
KULEEEE KOTE NI SHAMBA LETU: Kinana akimwambia Kinana wakati
akimuonyesha shamba hilo la alizeti ambalo limesaidia vijana wa kada
mbalimbali kujiajiri
Katibu
Mkuu, Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape (kushoto) wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na vijana wanaoshiriki
mradi huo wa kilimo cha alizeti, Iborogero wilayani Igunga mkoani
Tabora.
Mwenyekiti
wa Vijana SACCOS ya Igunga, Frey Cosseny (wapili kushoto)
akiwatambulisha kwa Kinana maofisa wengine wa SACCOS hiyo, Mei 9, 2014
alipofika kukagua shuguli za SACCOS hiyo na kuzungumza na wanachama.
Katibu Mkuu Kinana akiwasalimia wadau wa SACCOS hiyo
Kinana akiendesha trekta la mradi wa Igunga Vijana Saccos kulizindua
Kinana akishuka kwenye trekta baada ya kulizindua la Vijana SACCOS ya Igunga
Katibu
Mkuu Kinana akikabidhi funguo kwa mmoja wa Wana-SACCOS hiyo, Joseph
Kashindye, wakati alipokagua shughuli za SACCOS hiyo akiwa katika ziara
ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na
kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa wa Tabora, Mei 9, 2014.
(Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment