Mtaalamu
wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian
McClemen amewasili nchini leo alfajiri (Mei 4 mwaka huu) ambapo atakuwepo kwa
siku tatu.
McClemen
ameondoka leo (Mei 4 mwak huu) kwenda Bukoba ambapo atakagua Uwanja wa Kaitaba,
na kesho (Mei 5 mwaka huu) atakwenda jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.
Viwanja
hivyo vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa
Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClemen atatuma ripoti yake FIFA ili
shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa
Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni
Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na
Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment