Klabu
ya TP Mazembe imewaruhusu wachezaji wake Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu
kujiunga na timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo tayari imewasili Harare,
Zimbabwe kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika.
Taifa
Stars itacheza na Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mechi ya marudiano raundi
ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani
nchini Morocco. Mechi hiyo itachezwa Jumapili (Juni 1 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Harare.
Samata
na Ulimwengu watawasili Harare kesho (Mei 30 mwaka huu) saa 3.40 usiku kwa
ndege ya Kenya Airways. Watajiunga na TP Mazembe mara baada ya mchezo huo
ambapo Juni 2 mwaka huu watakwenda moja kwa moja Ndola, Zambia ambapo timu yao
imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment