Wakimbiaji
wakitimua vumbi katika mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon, mjini
Bagamoyo, Pwani jana. Mashindano hayo
yaliandaliwa na Kampuni ya 4Beli.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya
Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda (katikati) akihutubia wakati akifungunga mashindano ya Bagamoyo
Marathon mjini Bagamoyo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda (katikati) akimpongeza mshindi
wa mbio za kilomita 21 wanaume, Ismail Juma. Wengine ni baadhi ya washindi na
viongozi wa Kampuni ya 4Beli iliyoratibu mashindano hayo.
Mwakilishi wa Kampuni ya 4Beli akitoa zawadi kwa mmoja wa washiriki wa
mashindano.
Mwakilishi kutoka Benki ya Posta Tanzania (TPB) ambao walikuwa mmoja wa walidhamini
wa mashindano hayo akitoa zawadi kwa washindi.
No comments:
Post a Comment