Moja ya Bango la Hifadhi linavyotoa Ujumbe.
Tuwaunge Mkono TFS kwa kufuata yaliyoandikwa hapa.
Sehemu ya Barabara zilizomo ndani ya Hifadhi ya Misitu.
Maporomoko ya Maji yanayotokana na Hifadhi ya Bioanuwai ya Mlima Usambara Mashariki Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Sehemu ya Barabara zilizomo ndani ya Hifadhi ya Misitu.
Majani haya yanaajabu ukiyakamata yanasinyaa na kujifunga yapo katika ya Hifadhi ya Bioanuwai ya Mlima Usambara Mashariki Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Maporomoko ya Maji yanayotokana na Hifadhi ya Bioanuwai ya Mlima Usambara Mashariki Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Sehemu ya barabara zilizomo katika Hifadhi ya Misitu ya Bioanuwai ya Milima Usambara Mashariki Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Waandishi wakiwa katika Maporomoko ya maji yanayoelekea mto Zigi.
Huu ni mtego unaotumika kutegea Vipepeo katika Msitu wa Amani.
Watalii kutoka nchini Marekani wakijivinjali katika Misitu ya Amani wakihojiwa na waandishi wetu nchini.
Kundi la waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Habari waliofanya ziara ya kutembelea Hifadhi za Misitu Asilia zilizokuwa chini ya TFS.
Katika kiganja kuna Vitu kama majani ambayo ndani kuna Vipepeo wanaooteshwa na kuanguliwa kuna aina mbili ambazo ni Corax (kulia anauzwa kwa Tsh.750) na Padar kushoto anauzwa Tsh 1250 na kusafirishwa Marekani kwa shughuli mbalimbali za sherehe hasa wakati wa Ndoa
Ofisa Mkuu wa Hifadhi ya Misitu Asilia (TFS),Charles
Ng’atingwa, akionesha moja ya msitu wa Amani ya Hifadhi ya Bioanuwai ya Mlima Usambara Mashariki Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA
TAARIFA
YA HIFADHI YA MAZINGIRA ASILI CHOME
UTANGULIZI
Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia wa Chome
(Shengena) ni msitu wa Serikali Kuu unaosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania katika Wizara ya Maliasili na Utalii. Msitu huu ulitangazwa kwa mara
ya kwanza kuwa Msitu wa Hifadhi mwaka 1951 kwa tangazo la Serikali Na. 125 la
tarehe 25/05/1951. Ikafuatiwa na tamko la marekebisho kwa tangazo la Serikal Na
303 la tarehe 20/06/1958.
Hifadhi
hii ina ukubwa wa eneo la Ha 14,283 na
urefu wa mpaka wa Km 67. Hifadhi inazungukwa na vijiji 27 vilivyoko
katika kata 11.
Katika kuhakikisha kuna usimamizi mzuri Msitu
huu umegawanyika katika safu tano za usimamizi ambazo ni Chome, Suji, Mamba
miyamba, Bombo na Mbaga.
MALENGO
Kutokana na mpago kazi
wake hifadhi hii ina malengo yafuatayo:
1 Kutunza mazingira
asili, mfumo wa ikologia katika uasilia wake.
2 Kuimarisha uhifadhi
wa baianowai na mtawanyiko wake.
3 Kuimarisha mfumo wa
ekolojia.
4 Kulinda mmomonyoko
wa udongo na maporomoko ya ardhi na miamba.
5 Kuimarisha mafunzo
na tafiti mbalimbali.
6 Kushirikisha jamii
na wadau wote katika kulinda, kuhifadhi na kuendeleza uhifadhi.
7
Kuelimsha jamii inyozunguka hifadhi njia mbadala ya kupunguza umaskini.
HALI YA
AWALI YA HIFADHI
Hali ya Msitu huu ilikuwa na chnagamoto kubwa za
uhifadhi ambazo ni kama zifuatavyo;-
·
Uchimbaji
wa madini ndani ya hifadhi
·
Uchomaji
moto
·
Upasuaji
wa mbao
·
Uchungiji
wa mifugo
·
Ushiriki
mdogo wa wananchi katika kulinda hifadhi hii.
·
KUPADISHWA HADHI KUWA YA MAZINGIRA ASILIA
Kuna sababu nyingi za
kimsingi na za kitaalam zilizopelekea serikali kupandisha hadhi ya uhifadhi wa
misitu huo kuwa hifadhi ya mazingira asilia.
SABABU
HIZO NI KAMA IFUATAVYO:-
· Iligundulika
kuwa eneo hili lina bio-anuwai
nyingi za mimea na wanyama ambao ni
adimu, ndwele na wanaopatikana eneo hili tu.
· Eneo
hili linatunza maumbile ya asili na
kuboresha hali ya hewa na kuhifadhi gesi ukaa kuvuta mawingu yanayoleta
mvua za mara kwa mara.
·
Ni
tanki la maji kwa wakazi wanaozunguka hifadhi hii.
·
Ni
kivutio kwa watalii na hivyo utalii wa ekolojia unaendelezwa.
·
Ni
sehemu maalum kwa tafiti za ekolojia ya misitu ya tropiki.
HALI YA
HIFADHI BAADA KUPANDISHWA HADHI
Hatua hii ya kuupandisha Msitu na kuwa Hifadhi
ya mazingira asili kwa kiasi kikubwa imepunguza kwa kiasi kikubwa changamoto
zilizokuwa zinaikabili hifadhi hii ambapo shughuli za uchimbaji wa madini
zimepungua,kutoka watu zaidi ya 40 kwa siku na kuwa na wastani wa mtu mmoja
hadi 4 kwa siku.matukio ya moto yamepungua pamoja na mifugo. Wananchi wameelewa
umuhimu wa utunzaji wa hifadhi.
Ili kuhakikisha kuwa uhifadhi unaendelea na
hatimaye kufikia malengo tajwa hapo juu hifadhi hii inafanya shuguli zifuatazo;
·
Kufanya
Doria shirikishi ndani na nje ya Hifadhi kwa kushirikiana na kamati za
maliasili za vijiji
·
Kuimarisha
mpaka wa hifadhi kwa kusafisha na kupanda miti.
·
Kurejesha
maeneo yaliyoharibiwakwa kufukia mashimo yaliyoachwa wazi na wachimbaji madini
haramu, kurudisha mikondo ya maji kwenye njia za asili na kupanda miti
·
Kuandaa
na kusafisha njia za kitalii
·
Kuwasaidia
wanavijiji kuanzisha bustani za miti ya asili kwaajili ya kupanda mashambani
·
Kuwawezesha
wanavijiji wanazunguka hifadhi kuanzisha miradi midogomidogo ya kujiongezea
kipato mfano ufugaji nyuki,
·
Kuanzisha
Kamati za Maliasili za vijiji ili kuongeza ushiriki wa jamii zinazozunguka
hifadhi hii.
USHIRIKI
WA TAASISI NA MASHIRIKA MENGINE KATIKA UHIFADHI
Katika kuhakikisha kuwa hifadhi hii inatekeleza
majukumu yake kikamilifu hifadhi inashirikiana na taasisi na mashirika mbali
mbali kama;-
·
Ofisi
ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
·
Ofisi
ya mkuu wa wilaya Same
·
Ofisi
ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Same.
·
Ofisi
ya mkuu wa kituo cha polisi Same
·
Mfuko
wa hifadhi ya milima ya Tao la mashariki (EAMCEF)
·
Shirika
la Kuhifadhi Misitu Tanzania (TFCG)
·
Serikali
na halmashauri za vijiji
·
Wananchi
wanaozunguka hifadhi
MAFANIKIO
Kwa kushrikiana na wadau wengine pamoja na
serikali za vijiji mafanikio yafuatayo yamepatikana kipindi cha mwaka 2012 – 2014)
·
Kwa
kufanya doria shirikishi tumefanikiwa kuwaondoa wachimbaji wa madini ndani ya
hifadhi ambao walikuwa takribani 2000 na kufanikiwa kukamata zana mbalimbali
wanazotumia katika uchimbaji kama mashine za kusukumia maji (water pump) 20
Beleshi 30 Surulu10 n.k
·
Upasuaji
mbao umepungua ambapo kutokana na doria hizo misumeno 10 pamoja na wahalifu walikamatwa na kufikishwa
kwenye vyombo vya sheria pia mazao mbalimbali ya misitu yalikamatwa ikiwemo
milango 160 pamja na mbao vpande 100
·
Jumla
ya wahalifu 54 walikamatwa 16 kati yao wamehukumiwa vifungo vya kati ya mwaka
mmoja hadi miwili. 29 wamelipa faini 9 kesi zao bado zipo mahakamani.
·
Kuuongeza
ushiriki wa wananchi kwa kuanzisha Kamati za Maliasili za vijiji kwa kila
kijiji.ambazo jumla yao ni kamati 27.
·
Kuwaondoa
wavamizi wa hifadhi ambao walivamia kwa lengo la kulima au kuweka makazi ndani
ya hifadhi.
·
Kuimarisha
mpaka wa hifadhi kwa kupanda miti na kuweka mabango ili kuzuia uvamizi wa
hifadhi.
·
Kuwawezesha
wananchi kuanzisha bustani zao za miti ili kupanda katika mashamba yao.
·
Matukio
ya moto yaliyowahi kutokea yamepungua kutoka matukio 5 kwa mwaka hadi tukio
moja kwa siku.
·
Idadi
ya mifugo imezidi kupungua kutoka wastani wa ngombe 50 hadi wastani wa ngombe
watano wanaoingia ndani ya hifadhi.
CHANGAMOTO
·
Upungufu
wa rutuba katika mashamba ambao unasababisha jamii kutovuna mazao ya kutosha
kukidhi mahitaji yao.
·
Mtandao
wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu
hasa mbao zinazokamatwa na miti comphour(mkulo) kwa kutengenezea milango ,
vitanda n.k.
·
Kwa
ujumla wake ni matumizi dhidi ya uhifadhi.
No comments:
Post a Comment