Jeneza lenye mwili wa mtoto , Nasra Rashid
Mvungi ( 4)’ mtoto wa boksi’likiingizwa chumba cha kuhifadhi maiti.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya
Morogoro, wakiwemo Askari Polisi wa Kike, Waandishi wa Habari na
watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro katika Chumba
ya kuhifadhi maiti, wakishusha jeneza lenye mwili wa mtoto , Nasra Rashid
Mvungi ( 4)’ mtoto wa boksi’ aliyefariki juzi , Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Dar es Salaam , ulipowasili Juni 2 mjini hapa, mazishi yake
yatafanyika juni 3.
Jeneza likishushwa ndani ya gari.
Jeneza likishushwa ndani ya gari.
Baba mzazi wa mtoto Nasra , Rashid
Mvungi ( kati kati) akitafakari jambo , mara baada ya kuwasili mji Morogoro na
mwili wa mwanae ambao ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Juni 2, mtoto huyo
aliyefahamika kama 'mtoto wa boksi' alifariki dunia juni 1 katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili, Jijini Dar es Salaam, mazishi yanafanyika juni 3 makaburi ya Kola , Manispaa ya Morogoro.( Picha na John Nditi).
No comments:
Post a Comment