Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa
masikitiko kifo cha Mwakilishi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM)
katika Mkutano Mkuu wa TFF, William Chibura kilichotokea leo asubuhi (Juni 3
mwaka huu) katika Hospitali ya Mkoa wa Mara mjini Musoma.
Chibura aliyezaliwa mwaka 1969 alikuwa mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa TFF akiwakilisha klabu za Mkoa wa Mara kupitia FAM. Aliwahi
kuichezea Musoma Shooting, na baadaye kuwa kiongozi katika klabu hiyo na ile ya
Polisi Mara iliyoko Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Hadi mauti yanamkuta alikuwa kiongozi wa Butiama FC,
na mwakilishi wa klabu Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Butiama (MUFA) kwenye
Mkutano Mkuu wa FAM.
Msiba
huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini kwani, Chibura enzi za uhai
wake alitoa mchango mkubwa katika mchezo huu tangu akiwa mchezaji na baadaye
kiongozi.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Chibura, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Mara (FAM), Jeshi la Polisi Tanzania na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Taratibu
za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi Tanzania- Mkoa wa Mara, kwani marehemu Chibura alikuwa mtumishi wa jeshi
hilo. TFF tunasubiri taratibu hizo ili tujipange jinsi ya kushiriki katika
msiba huo.
Bwana
alitoa, na Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment