Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Dar es salaam.
Rais mstaafu wa awamu
ya pili , Ali Hassan Mwinyi ,amewataka watanzania kuwa makini kwa kutoruhusu
tofauti za dini zilizopo hapa nchini kuwa chanzo cha mgawanyiko miongoni mwao.
Kauli hiyo ameitoa jana
usiku jijini Dar es salaam wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki kwa
watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima, wananchi na viongozi
mbalimbali iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Mzee Ali Hassan Mwinyi
ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari hiyo amesema kuwa kila Mtanzania
bila kujadili itikadi na dini aliyonayo ana wajibu wa kulinda na kutunza amani
iliyopo kwa kuendelea kudumisha upendo na ukarimu kwa wenzake ikiwa ni sehemu
ya utekelezaji wa maagizo yaliyomo katika vitabu vitakatifu.
“Nawasihi Watanzania
wenzangu tuendelee kupendana, tuwe wamoja katika kushirikiana, kamwe tusiruhusu
wala kukubali mgawanyiko wa dini wala itikadi zetu” Amesisitiza.
Amewashukuru viongozi
wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Saidi Meck Sadiki kwa
uamuzi walioufanya wa kuandaa Futari iliyowaunganisha watoto yatima, wananchi
na viongozi mbalimbali bila kujadili itikadi
na dini zao ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu walio nao.
Kwa upande wake Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza wakati wa Futari hiyo aliyowaandalia
wageni hao amesema kuwa serikali ya mkoa inaendelea
kutekeleza mipango mbalimbali ya
maendeleo ikiwemo ukarabati na ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya wakati
wa msimu wa mvua jijini Dar es salaam.
Bw. Sadiki ameziagiza
Halimashauri za Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni na Wakala wa Barabara (TANROAD) mkoa wa Dar
es salaam kuhakikisha kuwa wanarejesha hali ya kupitika kwa barabara
iliyokuwepo mwanzo ili kuwaondolea kero ya usafiri wananchi.
Naye Sheikh Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Sheikh Alhadi Mussa Salum
akuzungumza wakati wa Futari hiyo ameeleza kuwa viongozi wa dini na serikali
kote nchini wanalo jukumu kubwa la kuwaongoza wananchi kutenda mema na
kuendelea kuvumilia.
Amezitaka mamlaka hizo
kutumia fedha za ndani na zile zilizotolewa na Serikali Kuu kukamilisha
ukarabati wa miundombinu hiyo yakiwemo madaraja
yaliyosombwa na maji kwa muda muafaka ili kuruhusu magari kuweza kufika katika
maeneo hayo.
Katika hatua nyingine
Bw. Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kushiriki
kikamilifu katika suala la usafi na uhifadhi wa mazingira kwa kujenga utaratibu
wa kusafisha mazingira ya jiji ili kulinda heshima ya jiji huku akisisitiza
kuwa dini zote zinamtaka mwanadamu awe mwadilifu na mwenye kuzingatia usafi.
Amezitaka mamlaka
zinazosimamia utekelezaji wa sheria za kuhifadhi mazingira jijini Dar es salaam
kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuhakikisha maeneo yote ya jiji
yanaendelea kuwa katika hali ya usafi.
Baadhi watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya
kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam wakijumuika pamoja katika Futari
iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki.
Rais mstaafu wa Awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye
alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam kwa watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya
jiji la Dar es salaam akijumuika pamoja na watoto hao na wageni mbalimbali walioalikwa
katika Futari hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (kushoto) na Mkuu wa Mkoa
wa Songea Dkt. Christine Ishengoma(kulia) wakiungana na viongozi wengine kushiriki Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam kwa watoto yatima kutoka katika vituo mbalimbali katika viwanja vya
Karimjee jijini Dar es salaam.
Rais wa
Tanzania wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati
wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akisisitiza umuhimu wa kulinda na kutunza amani
iliyopo kwa kuendelea kudumisha upendo na ukarimu ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa maagizo yaliyomo katika vitabu vitakatifu.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (kushoto) na Mkuu wa Mkoa
wa Songea Dkt. Christine Ishengoma(kulia) wakiungana na viongozi wengine kushiriki Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam kwa watoto yatima kutoka katika vituo mbalimbali katika viwanja vya
Karimjee jijini Dar es salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akiongea na watoto wanaotoka katika
vituo mbalimbali vya kulelea watoto
yatima vya jijini Dar es salaam , wakazi
wa jiji la Dar es salaam na viongozi mbalimbali wakati wa Futari aliyooiandaa
jana usiku katika viwanja vya Karimjee.
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika viwanja vya
Karimjee kuhudhuria Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi
Meck Sadiki (wa pili kutoka kushoto) kwa watoto yatima kutoka vituo mbalimbali
vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam. Wengine wanaoonekana kutoka
kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum.
Baadhi ya akina mama waliohudhuria Futari hiyo wakipata Chakula.
Baadhi ya
watoto waliohudhuria Futari hiyo wakipata Chakula.
Kamanda
wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova (katikati) akifafanua
jambo kwa viongozi wa mkoa wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck
Sadiki (wa pili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi(kulia)
na Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia
Mjema (kushoto) wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa huo katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Mkuu wa
wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw.
Raymond Mushi(kulia) na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna
Suleiman Kova (wa pili kutoka kushoto) wakati
wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam katika viwanja vya
Karimjee jijini Dar es salaam.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum (wa kwanza kushoto) na Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahmani Kinana wakijumuika katika Futari hiyo.(Picha
na Aron Msigwa- MAELEZO).
No comments:
Post a Comment