KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Thursday, August 14, 2014

AJALI KWA WANAJESHI ILIYOSABABISHA VIFO.




JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E            Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463      Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                        DAR ES SALAAM, 13 Agosti, 2014
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa masikitiko makubwa linapenda kuwatangazia Wananchi wote kuwa mnamo tarehe 11 Agosti, 2014 muda wa saa 11:30 jioni Askari wa JWTZ wakiwa na gari lenye Nambari UN 47089 aina ya Leyland Ashock likiwa kwenye msafara kutoka Beni kuelekea Sake, limepata ajali maeneo kati ya Rwindi na Kanyabayoga nchi DRC.

Gari hilo lilikuwa na Askari idadi watano (5) miongoni mwao Askari watatu (3) walifariki dunia papo hapo.  Askari waliofariki ni kama ifuatavyo:-

a.       Private Mohamed John Mbizi.
b.       Private Vasco Adrian Msigala.
c.        Private Ally Salum Jumanne.

Askari idadi wawili (2) walipata majeraha,  ambao wamechukuliwa na helicopter kwenda Goma kwa matibabu zaidi.  Majina yao ni kama ifuatavyo:-








a.        Private Emily Edward Lyombe
b.        Private Haji Hassan Amme

Kuwasili kwa miili ya marehemu na taratibu za maziko zitatolewa baadae.




Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0754  270136

No comments: