JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA
HABARI NA MAHUSIANO
Simu ya Upepo : “N
G O M E” Makao Makuu ya
Jeshi,
Simu ya Mdomo :
DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex
: 41051 DAR
ES SALAAM, 14 Agosti, 2014
Tele Fax
: 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), linatarajia kuzindua huduma ya Tiba kwa
jamii kuanzia tarehe 15 Agosti 2014 hadi 19 Agosti 2014 kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi
12:00 jioni katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Huduma hizi zinakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya JWTZ.
Huduma
zitakazotolewa ni pamoja na vipimo vya magonjwa ya Homa ya Ini (Hepatitis
B& C), Presha, Kisukari, Huduma za Ushauri nasaha na kupima VVU, Huduma za
uchangia damu salama, Macho, Kinywa na Koo.
Kwa vipimo vya Malaria, matibabu yatatolewa hapo hapo. Huduma zote hizo ni bure.
Nafasi
hii itatoa mwanga wa kuweza kuona ueledi wa madakitari wetu wazalendo ambao ni
matunda yenu.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya Dk Selemani Seif
Rashidi. JWTZ linawakaribisha wananchi
wote.
Tumelinda, tunalinda, tutalinda daima Taifa
letu Tanzania.
Imetolewa na Kurugenzi
ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0754 -
270136
No comments:
Post a Comment