Mke wa Rais
na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete
akipokewa na Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Watanzania
wanaoishi Washington kiitwacho TANO Ladies Ndugu Asha Hariz wakati
alipotembelea ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kipeperushi
kutoka kwa Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya
Help for Underserved Communities
(HUC) ya nchini Marekani Ndugu Zawadi Sakapalla baada ya kupata taarifa
ya huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo. Kampuni hiyo husaidia familia
maskini kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa kuwachimbia visima
pamoja na kutoa vifaa vya elimu kwa wanafunzi.
Baada ya kutembelea maonesho ya wanawake
wajasiriamali Mama Salma Kikwete akifuatana na Afisa Tawala wa Ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka kwenda kuweka saini kwenye kitabu
cha wageni.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye
kitabu cha wageni. Aliyesimama kushoto ni Bibi Lily Munanka, Afisa wa Ubalozi
wa Tanzania nchini Marekani.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akitambulishwa kwa wana kikundi wa TANO Ladies. Wa kwanza
kushoto ni Mwenyekiti Asha Hariz, akifuatiwa na Asha Nyang’anyi, Isca Kauga,
Juster Mutakyawa na Tumaini Kaisi aliyeshika kipaza sauti.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kikundi cha TANO Ladies cha nchini
Marekani. Anayekabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya wanakikundi wenzake Ndugu Juster
Mutakyawa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani
kwenye ukumbi wa ofisi ya ubalozi wetu mjini Washington.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani
kwenye ukumbi wa ofisi ya ubalozi wetu mjini Washington.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani
kwenye ukumbi wa ofisi ya ubalozi wetu mjini Washington.
Baadhi ya wanawake wajasiriamali na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na baadhi
ya wanawake mwishoni mwa mazungumzo yake na wanawake hao yaliyofanyika kwenye
ukumbi wa ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani huko Washington.
Mke wa Rais
akipiga picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa
Liberata Mulamula.
Balozi wa
Tanzania nchni Marekani Mheshimiwa Liberata
Mulamula akimuaga Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya
kutembelea ofisi za ubalozi huo na kuongea na wanawake wa Tanzania wanaoishi
nchini Marekani.(PICHA NA JOHN LUKUWI).
No comments:
Post a Comment