Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa
Filamu ya The Minister katika hafla iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es
Salaam, anayeshuhudia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce
Fissoo.
Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akifurahia mara baada ya kukata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Filamu ya The Minister katika hafla iliyofanyika
hivi karibuni jijini Dar es Salaa,. Filamu hiyo imetengenezwa na Kampuni ya
Equity Link Enterpreses ya jijini Dar es Salaam ambapo inaelezea namna viongozi
wa umma wanavo ishi katika muktadha wa maadili miongoni mwa jamii zao.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzaia Bibi
Joyce Fissoo akimpongeza Jaji Mstaafu Salome Kaganda mara baada ya kuzindua
rasmi Filamu ya “The Minister” Filamu hiyo ilimetengenezwa na Kampuni ya Equity
Link Enterpreses ya jijini Dar es Salaam inaelezea namna viongozi wa umma
ambavyo utumia nyadhifa zao bila kuzingatia maadili.Katika ni Muongozaji Mkuu
wa Filamu hiyo na Mkurugenzi wa Kampuni iliyotengeneza Filamu hii Bibi. Deborah
Nyakirang’ani.
Msaani wa Filamu mbaye ameigiza kama Mhe. Waziri
katika filamu hiyo Bw. Julius Busee (Mr.Kakula) akifanya mahojihano na
waandishi wa Habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Filamu ya “The Minister”
ambapo yeye ndiyo muhusika mkuu.
Katikati Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akiangalia ngoma mara baada ya
kuzindua rasmi Filamu ya The Minister jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na kulia ni Muongozaji
Mkuu wa Filamu hiyo na Mkurugenzi wa Kampuni iliyotengeneza Filamu hii Bibi.
Deborah Nyakirang’ani.
Wa kwanza kutoka kulia Mkurugenzi wa Msaidizi wa Utamaduni kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Leah Kihumbi akiwa na
baadhi ya wadau wa Filamu wakiangalia Filamu The Minsiter ilipoonyeshwa kwa
mara ya kwanza wakati wa hafla za uzinduzi wake hivi karibuni katika Ukumbi wa
Century Cinemax jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzaia Bibi Joyce
Fissoo akiwa katika picha ya pamaoja na wasanii walioigiza akatika Filamu ya
The Minsiter mara baada ya uzinduzi kukamilika, Filamu hiyo imetengenezwa na
Kampuni ya Equity Link Enterpreses ya jijini Dar es Salaam ambapo inaelezea
namna viongozi wa umma wanavo ishi katika muktadha wa maadili miongoni mwa
jamii zao.
(Picha zote na Frank Shija - WHVUM)
Na Frank Shija, WHVUM
Viongozi wa umma wametakiwa kuendeleza uzalendo ambao muasisi wa Taifa hili Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere alituachia.
Rai
hiyo himetolewa na Kamishna wa Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda alipokuwa
akizindua Filamu ya "The Minister" mapema hivi karibuni jijini Dar es
Salaam.
Jaji
Kaganda alisema kuwa viongozi wanapaswa kuwa mstari wa mbele
kuhakikisha uzalendo unakua hapa nchini ikiwa ni pamoja na kufanya kazi
kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria badala
ya kuendelea kupiga kelele bila vitendo.
Aidha
Jaji Kaganda aliongeza kuwa watumishi wa umma wanaongozwa na kanuni za
maadi ya utendaji ambapo alitaja sheria ya maadili ya viongozi wa Umma
Na. 13 ya mwaka 1995 na kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma za mwaka
2005 ambapo alisema mtumishi akizingatia ni dhahiri kwamba atakuwa
mzalendo wa kweli.
Aliongeza
kuwa amefarijika kuona wasaniisasa wameamua kutumia
vipaji vyao kutoa Elimu ya maadili ambapo kupitia Filamu ya The
Minister viongozi wengi watajifunza ana kujisahihisha pale walipoteleza.
Alisema Jaji Kaganda
Jaji
amesema kuwa maadili ni suala nyetu kwani bila maadili haki haipatikani
hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kwa nafasi yake kuhakikisha
kunajenga jamii yenye maadili.
Katika
hali ya kuonyesha amevutiwa na Filamu hiyo Jaji Kaganga ametangaza
rasmi kuwa Ofisi yake itatumia Filamu hiyo kama kielelezo rasmi wakati
wa utekelezaji wa shughuli za uelimishaji kwa umma.
"
Nimefurahishwa sana na maudhui ya Filamu hii naomba nipatiwe nakala
angalau tano hili nami niweze kuwa na vielezo vya kutumia pindi
tunapotekeleza majukumu yetu ya kuelemisha umma juu ya maadili ya
viongozi" Alisema Jaji Kaganda.
Kwa
upande wake Muongozaji wa Filamu hiyo na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Equity Link Enterprises Bibi. Debora Nyakirang'ani amesema kuwa wazo
hilo la Filamu ya The Minister baada ya kubaini kuwa wasanii wengi
ujikita zaidi katika kucheza filamu zenye mafundisho tofauti na kusahau
eneo nyeti la maadili.
Kushuka
kwa maadili miongoni mwa jamii imekuwa ni chachu ya vijana wengi
kutokuwa wazalendo wa nchini yao tena badala yake watu wamebaki kuwa
wabinafsi zaidi.Hivyo nimatarajia yangu kwamba kupitia Filamu hii wwatu
watabadilika na kurudu katika mstari ulionyooka. Alisema Bibi.
Nyakarang'ani.
Filamu
ya The Minister ni filamu ya kitanzania iliyoandaliwa na kutengenezwa
na Kampuni ya Equity Link Enterprises,katika Filamu hiyo inaelezea namna
mhusika mkuu
alivyobadilika ghafla mara baada ya kupata wadhifa wa Uwaziri, na jinsi
ambavyo alikuwa akiishi katika maisha yake binafsi yakionyesha
azingatii maadili yake ya kazi ipasavyo.
No comments:
Post a Comment