KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Wednesday, September 10, 2014

Mwenyekiti wa WAMA Mke wa Rais Mama Salma Kikwete afanya ziara ya kutembelea Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Dar es Salaam.

 Sehemu ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
 Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akipokewa na mwenyeji wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bohari Kuu ya Dawa (MSD),Cosmas Mwaifwani (kulia),Meneja  huduma kwa Wateja,Salome Mallamia na wengine.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bohari Kuu ya Dawa (MSD),Cosmas Mwaifwani (wapili kushoto) akimtambulisha Mama Salma, Meneja  Huduma kwa Wateja,Salome Mallamia na Mkurugenzi wa Ugavi, Missanga Muja (kulia).
 Mwenyekitui wa WAMA Mama Salma akitambulishwa viongozi wa (MSD)
  Mwenyekitui wa WAMA Mama Salma akitambulishwa viongozi wa (MSD)
  Mwenyekiti wa WAMA mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembezwa katika ghara la kuhifadhia Dawa na mwenyeji wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bohari Kuu ya Dawa (MSD),Cosmas Mwaifwani.
  Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akpewa maelezo na mwenyeji wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bohari Kuu ya Dawa (MSD),Cosmas Mwaifwani.
  Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akioneshwa baadhi ya vifaa na Ofisa Mauzo MSD,Yonah Msengi.huku watu wengine wakishuhudia wakati wa ziara hiyo.
  Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akigusa moja ya bosi lenye dawa.
 Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya kipimio cha uzito wa mtoto baada ya kuzaliwa cha digito  kutoka kwa Ofisa mauzo wa Bohari ya Dawa (MSD),Yonah Msengi (kulia) Mama alitembelea Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kuangalia vifaa vya akina mama vinavyotumika katika kujifungua. Wengine Kaimu Mkurugenzi Mkuu Cosmas Mwaifwani (katikati) na viongozi wengine.
 Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia moja ya shuka alipotembelea Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia vifaa vya akina mama vinavyotumika wakati wa kujifungua. Kushoto Ofisa Mauzo Yonaha Msengi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Cosmas Mwaifwani (katikati). 
 Sehemu ya Mabosi yaliyojaa Dawa Bohari Kuu (MSD) Jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Mabosi yaliyojaa Dawa Bohari Kuu (MSD) Jijini Dar es Salaam.Hakuna shida ya Dawa.
 Mwenyekiti wa WAMA akiangalia Dawa ndani ya Ghara.
  Mwenyekiti wa WAMA akiangalia Dawa ndani ya Ghara.
 Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akioneshwa vifaa vya kina mama na  Ofisa Mauzo Yonaha Msengi.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akiangalia vifaa vinavyotumika na akinamama wakati wa kujifungua alipofanya ziara Bohari Kuu ya Dawa Jijini Dar es Salaam.

WAJAWAZITO WAKIJIFUNGUA KATIKA MAZINGIRA SALAMA VIFO VYAO VITAPUNGUA - SALMA KIKWETE

 Na Anna Nkinda – Maelezo
Ili kuhakikisha vifo vya kina mama wajawazito vinapungua ni lazima wajifungue katika mazingira salama huku kukiwa na upatikanaji wa kutosha wa vifaa tiba.


Hayo yamesemwa jana na Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Mama Salma Kikwete wakati akiongea na viongozi wa Bohari ya Dawa (MSD) iliyopo Keko Jijini Dar es Salaam.


Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alitembelea makao makuu ya MSD kwa ajili ya kuangalia vifaa tiba ikiwa ni pamoja na vifaa vya kujifungulia  kina mama wajawazito.


Alisema kama mama atajifungua katika mazingira salama nchi itaweza kuvuka malengo ya milinia ya kupunguza vifo vya kina mama wajawazito ambavyo kwa sasa vimepungua kutoka 452 kwa kila vizazi hai 100000 hadi kufikia 432 kwa kila vizazi hai 100000 jambo ambalo litasababisha maisha ya mama kuwa bora.


“Moja ya kazi zinazofanywa na taasisi ya WAMA ni kuboresha afya ya mama na mtoto hapa nchini, katika hili tunatoa vifaa tiba vikiwemo vitanda vya kujifungulia kina mama wajawazito katika Hospitali, vituo vya Afya na Zahanati  ili kuhakikisha kina mama wanajifungua katika mazingira salama” .


Wakati wa ziara ya Rais Kikwete  mkoani Morogoro niliahidi kutoa vitanda vya kujifungulia ili kina mama waweze kujifungua salama, nimekuja hapa na nimejionea vitanda vizuri na vya kisasa vya kujifungulia pamoja na vifaa vingine ambavyo vinatumika kwa mama mjamzito naahidi nitawapelekea vifaa hivyo”, alisema Mama Kikwete.


Aidha Mama Kikwete pia aliwataka viongozi hao kuongeza juhudi  katika utendaji wao wa kazi  ya kuokoa maisha ya binadamu na kuhakikisha dawa wanazozipokea zinafika kwa mlaji kwa wakati kwani kama zitafika kwa wakati vifo vitapungua.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD Cosmas Mwaifwani alisema tangu mwaka wa fedha uliopita wameanza kupeleka dawa na vifaa tiba moja kwa moja katika ngazi ya vituo vya afya na kuvifikisha kwa mlaji nia ikiwa ni kufikisha huduma hii kwa mlengwa kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati.


“Dhina ya MSD ni  kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba vyenye ubora kwa bei naafuu kwa watanzania wote, ndiyo maana tunafika Tanzania nzima na hata kule ambako kuna ugumu wa kufika zinaangaliwa njia mbadala za kufika huko”.


Hivi sasa tunaweza kusimama na kuizungumzia dhina hii bila wasiwasi kwani kwa sasa tafiti zinaonyesha kuwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeongezeka kutoka asilimia 45 hadi kufikia asilimia 85”, alisema Mwaifwani.


Alisema pamoja na kwamba MSD inashughulikia Hospital, Zahanati na Vituo vya afya vya Serikali na taasisi zilizoidhinishwa na wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii bado ipo tayari kutoa huduma kwa  makundi mengine ambayo yanatuma maombi kwa ajili ya kununua vifaa tiba kwa matumizi ya wananchi.


Mwaifwani alisema, “Pale ambapo kundi la watu ama mtu binafsi anapohitaji vifaa tiba kwa ajili ya matumizi ya wananchi na vifaa hivyo vikiwepo MSD, hatutakuwa na hiyana ya kutompatia huduma hiyo kwani tumedhamiria kuokoa maisha ya watanzania”.


Bohari ya Dawa ni moja ya Idara inayojitegemea chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inajiendsha chini ya Bodi ya wadhamini yenye majukumu makuu matatu ambayo ni kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa Hospitali za Serikali na zile zilizoidhinishwa na wizara.

No comments: