JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA
HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N
G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo :
DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex
: 41051 DAR ES SALAAM, 30 Oktoba, 2014
Tele Fax
: 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa ya kifo kwa Vyombo vya Habari
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis
Mwamunyange anasikitika kutangaza kifo cha Meja
Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) kilichotokea tarehe 29 Oktoba 2014 katika
Hospitali ya Appolo nchini India alikokuwa akipata matibabu.
Mwili wa marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse
(mstaafu) unatarajia kuwasili Tanzania tarehe 31 Oktoba 2014 saa 7:30 mchana na
kuhifadhiwa katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo.
Heshima za mwisho kwa Viongozi, Wanajeshi na Watumishi
wa Umma zitatolewa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 01 Novemba 2014, kuanzia saa
4.00 hadi saa 5.00 asubuhi na mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Njombe kwa
mazishi, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba, 2014 saa 8.00 mchana.
Imetolewa na Kurugenzi
ya Habari na
Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 -
309963
No comments:
Post a Comment