KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Thursday, January 22, 2015

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA CBE.

 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema (wa pili kutoka kulia) akimtambulisha viongozi wa chuo cha CBE ,Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd (katikati) leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akipata maelezo kutoka kwa  Bi. Esther Kibua, mwanafunzi wa mwaka wa 3 wa chuo cha Elimu ya Biashara CBE kampasi ya Dar es salaam juu ya namna chuo hicho kinavyowaandaa kuitumia elimu wanayoipata chuoni hapo pindi watakapomaliza masomo yao.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimuuliza swali Bi. Esther  Kibua, mwanafunzi wa mwaka wa 3 wa chuo cha Elimu ya Biashara CBE kampasi ya Dar es salaam  alipotembelea banda la maonesho la wanafunzi wa Chuo cha CBE jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za  kilele cha miaka 50 ya chuo hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akifafanua akifafanua jambo alipotembelea banda la maonesho la Idara ya Mizani na Vipimo la Chuo cha CBE jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za  kilele cha miaka 50 ya chuo hicho.Kushoto ni Mwalimu wa Idara ya Mizani na Vipimo wa Chuo hicho Bw. Faraja Nyoni.(Picha na Aron Msigwa –MAELEZO).

No comments: